Ushauri wa kisheria kuhusu mkataba huu niliosaini

isackjr

Member
Joined
Sep 16, 2016
Posts
20
Reaction score
10
Habari wana JamiiForums,

Nilikuwa naomba ushauri wenu.

Kuna company nilipata kazi wakanipa mpaka mkataba nikasaini ila siku ya kuanza kazi haikupangwa kutoka na kutojua siku sahihi ya kufungua hiyo company.

Kilichokuja kutokea baada ya kuwatafuta sana kwenye simu na email bila majibu ikabidi niende ofisini kwao, nikashia nje bila kumuona HR walinzi walikataa kuniruhusu kuingia ikabidi nimtafute kwa simu akawa hapokei.

Akaja kupokea baadae baada ya kupiga sana kwa masaa zaidi ya manne, akaniambia walinitafuta kwa njia ya simu wakanikosa kazi wameshampa mtu mwingine.
 
Jambo lako lina utata sana.
Huo mkataba wako uliosaini ulikuwa ni wa aina gani labda ili tupate utatuzi wake.
Na je baada ya kusaini mkataba ulikuwa unaingiziwa mshahara kila mwezi?
Maana ninavyojua Mimi mkataba lazima uandikwe siku unaoanza na siku ya kumalizika,je mkataba uliandikwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…