Mimi ni mjumbe wa baraza la usuluhishi la ukoo wa kichaga,na alitokea kijana fulani ambae alizaa na mke wa mtu,baada ya muda mchache yule kijana akafariki lakini yule mwenye mke akaficha siri kuondoa aibu. Muda ulivyozidi kwenda yule mtoto akakua na akapata mume wa kumuoa lakini kila akipata ujauzito akizaa mtoto akawa anakufa katika kutafuta tatizo ikagundulika kuwa mtoto alikua anahitajika kutmbulishwa kwenye upande wa baba yake mzazi ambae alikua ni marehemu,hivyo taarifa zikatumwa kwa familia ya marehemu baba yake kusikia kua marehemu anamtoto ndugu wa marehemu wakagawana shamba haraka ili huyo mtoto asipate kitu lakini tetesi zikavuja nakufikia ukoo. Swali langu ni hili, kwa mazingira haya huyu mtoto anahaki kisheria kudai haki ya marehemu baba yake? Na nimewatega hawa wanafamilia kwa swali hili,je wanamtambua na kumkubali huyu mtoto kuwa ni wa ndugu yao wamekubali lakini wanasema kwao mtoto wa kike hana urithi wa shamba. Naomba ushauri wenu wa kisheria ili kumsaidia huyu mtoto pia kubadili fikra za jamii hii ya kichaga kuhusu mtoto wa kike. Na wasilisha