Ushauri wa kisheria kuhusu urithi!

Ushauri wa kisheria kuhusu urithi!

Chasaka

Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
67
Reaction score
14
Mimi ni mjumbe wa baraza la usuluhishi la ukoo wa kichaga,na alitokea kijana fulani ambae alizaa na mke wa mtu,baada ya muda mchache yule kijana akafariki lakini yule mwenye mke akaficha siri kuondoa aibu. Muda ulivyozidi kwenda yule mtoto akakua na akapata mume wa kumuoa lakini kila akipata ujauzito akizaa mtoto akawa anakufa katika kutafuta tatizo ikagundulika kuwa mtoto alikua anahitajika kutmbulishwa kwenye upande wa baba yake mzazi ambae alikua ni marehemu,hivyo taarifa zikatumwa kwa familia ya marehemu baba yake kusikia kua marehemu anamtoto ndugu wa marehemu wakagawana shamba haraka ili huyo mtoto asipate kitu lakini tetesi zikavuja nakufikia ukoo. Swali langu ni hili, kwa mazingira haya huyu mtoto anahaki kisheria kudai haki ya marehemu baba yake? Na nimewatega hawa wanafamilia kwa swali hili,je wanamtambua na kumkubali huyu mtoto kuwa ni wa ndugu yao wamekubali lakini wanasema kwao mtoto wa kike hana urithi wa shamba. Naomba ushauri wenu wa kisheria ili kumsaidia huyu mtoto pia kubadili fikra za jamii hii ya kichaga kuhusu mtoto wa kike. Na wasilisha
 
sijajua kama hao watu wanao uhakika/ushahidi asilimia 100% kwamba mtoto huyo ni wa kambo. ushahidi gani wanao? kama ni hisia tu, hizo hazitambuliki kisheria. nafikiri ungeeleza kwanza namna gani wana uhakika na ushahidi huo ndipo tutapata, na namna gani wewe mwenyewe una uhakika na jambo hilo kama la kweli ama la.

HUYO MTOTO HATARITHI mali za marehemu baba yake ambaye amekufa bila kumtambulisha/kumhalalisha, labda kama alikuwa amemwandika kwenye wosia.....hapo kama kweli imethibitika yeye ni mtoto wa kambo, hatakuwa na haki kurithi kwa sheria za mirathi ya kimila na hata kiserikali au kiislam. hatakiwi kurithi; ila hapo ATAKUJA KURITHI MALI ZA MAMA YAKE AKIFA, mali za marehemu baba yake ambaye amekufa bila kumtambulisha/kumhalalisha na kutambulika kuwa wake, hatakiwi kurithi. huyo mtoto hana haki hiyo....labda kama atakuwa aliandikwa kwenye wosia kama mtu baki tu na si kama mtoto.

TUNAHALALISHAJE WATOTO/TUNAWATAMBULISHAJE?...Kuna mila tofautitofauti, makabilia mengine huwa wanaweza kulipa fungu la fedha wanapojitambulisha, weninge ng'ombe, wengine wanaenda tu na washenga kujitambulisha kwa wazazi wa mwanamke waliyemzalisha...na kwa huyo ambaye mwanamke alikuwa anatoka nje ya ndoa hata mtoto wa kambo akatokea lazima kikao cha ukoo kingekaliwa na kupigana faini na mambo kama hayo hata mtoto huyo aliyezaliwa ndani ya ndoa lakini ni wa kambo atambulishwe baba yake ni yupi.bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI

View attachment 104019

View attachment 104020View attachment 104020View attachment 104020View attachment 104020
 
Huyu mtoto kazaliwa ndani ya ndoa ya mtu, baba yake kamzalisha mke wa mtu,na babake alifariki kabla hajaoa hivyo mtoto wake pekee ndie huyu msichana aliyezaa na mke wa mtu,na babake wakambo kamleta kwa ndugu za babake halisi waliodhulumu ni hawa ndugu wa babake halisi na kudai mtoto wakike hanaurithi wakati babake alikuwa na shamba.
 
Sioni kwanini arithi....huyo hajikani kisheia
 
tafuta wanasheria. kuna kitabu wanakitangaza sana humu ndani, nimedownload na kuattach hapa
 
Back
Top Bottom