Ushauri wa kitaalam

Ushauri wa kitaalam

MKWANO

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2014
Posts
230
Reaction score
159
Amani iwe Kwenu wapendwa, jana nilitembelewa na jamaa angu akiomba ushauri.

Alikuwa amekopa mkopo bank miezi 6 iliyopita, sasa kuna asasi ya mikopo eti inataka kununua deni alilokopa bank . Sasa amekuja kwangu ili kujua faida kwake ni ipi kama jamaa watanunua kweli hili deni, na hasara kama zipo, nami sio mtaalamu wa haya masuala.

Mwenye utaalamu tafadhali.
 
watanunua lakin atalilipa kwa riba kubwa zaidi tena kwa kipindi kifupi.

huyo anabebeshwa mzigo wa msumari tu bora alipe mwenyewe bank.Asipofanya hivyo ajiandae kwa presha na kufilisiwa hizi taasisi za mkopo hazina huruma wala cha mswalie..........
 
Kwa mantiki hiyo ni bora asubiri mda upite kidogo alafu aka renew mkopo bank, maana anatafuta ada aende masomo.
 
Amani iwe Kwenu wapendwa, jana nilitembelewa na jamaa angu akiomba ushauri.

Alikuwa amekopa mkopo bank miezi 6 iliyopita, sasa kuna asasi ya mikopo eti inataka kununua deni alilokopa bank . Sasa amekuja kwangu ili kujua faida kwake ni ipi kama jamaa watanunua kweli hili deni, na hasara kama zipo, nami sio mtaalamu wa haya masuala.

Mwenye utaalamu tafadhali.
haya ni masuala ya namba mkuu. Inakuwa vigumu kutoa ushauri bila kujua vitu kama interest, kiwango cha mkopo, muda wa kulipa, penalty ya kusitisha mkataba, monthly charges, other benefits etc.
 
Back
Top Bottom