Enny
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 962
- 130
Hamjambo wana JF. Naomba ushauri, mimi nafanya kazi kampuni fulani nje ya Dar na familia yangu ipo Dar. Huwa napata likizo kila baada ya miezi mitatu. Mshahara wake ni mzuri. Nimepata kazi Dar ili nikae na familia yangu ingawa mshahara si mkubwa. Kwa hilo nimeridhika. Ila nafikiria namna ya kumwambia bosi wangu hapa kuwa naacha kwani ni muda wa mwezi nilifikiria kuacha akanibembeleza niendelee nami nikakubali hapo nilikuwa sina kazi. lakini baada ya wiki mbili nikajulishwa kuwa nimpata kazi. Nisaidieni mawazo namna ya kumwambia bosi wangu wa sasa ili nitoke kwa amani hapa,