Ushauri wa kujenga

Ushauri wa kujenga

buyoya419

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Posts
618
Reaction score
498
Habari zenu,

Nataka nianze kujenga ila mdogomdogo.

Kuna ramani nitaituma hapo ndio nataka nyumba yangu iwe hivyo ila nitaanza na chumba kimoja kimoja mpaka inaisha.

Lengo langu ni kujenga msingi kwa wakati mmoja ila kupandisha juu nitaanza na chumba kimoja kimoja.

Wataalamu nataka nifahamu gharama ya kuhudumia msingi mpaka ukaisha tofari ngapi zinahitajika, cement n.k

IMG-20230703-WA0002.jpg
 
Andaa 10M ya haraka hapo unainua hio nyumba mkuu, utafikia level nzuri sana, though vinaweza baki vitu vichache kukamilisha
 
Ila kama tayari una kiwanja mpaka kuifikisha hio level unafika kwa 5-7 hivi
 
Ila kama tayari una kiwanja mpaka kuifikisha hio level unafika kwa 5-7 hivi
Lengo langu ni kwenda kwa awamu,maana sitaweza kuinua kwa wakati mmoja kwa kazi zetu hizi ambazo hazieleweki

Awamu nilizopanga ni hizi
1.Msingi wote
2.Kuipandisha mpaka kwenye lenta
3.Kupiga lenta
4.Kuimalizia mpaka mwisho wa tofari
 
Majibu kumbe unayo alaf umekuja kutuchora😁😁
 
Kwa msingi pekee kwa mfumo wa ramani hiyo andaa:-
1: Tofari kama 700@1 Sh.1000x700 = 700,000/=
2: Simenti mifuko 15 @1 Sh.15,500x15 = 232,500/=
3: Nondo 7 za rinta ya Msingi @1 Sh 20,000x7 = 140,000/=
4: Kokoto kama Ndoo 50 @1 sh.4000x50 = 200,000/=
5: Mchanga Canter 1 @ 240,000 = 240,00/=
6: Pesa ya Fund sio chini ya 500,000/=
7: Weka na pesa ya Maji site hapo kama 100,000/=
Halafu jumlisha pesa ngapi hapo msingi tu unaisha saafi!
 
Habari zenu,

Nataka nianze kujenga ila mdogomdogo.

Kuna ramani nitaituma hapo ndio nataka nyumba yangu iwe hivyo ila nitaanza na chumba kimoja kimoja mpaka inaisha.

Lengo langu ni kujenga msingi kwa wakati mmoja ila kupandisha juu nitaanza na chumba kimoja kimoja.

Wataalamu nataka nifahamu gharama ya kuhudumia msingi mpaka ukaisha tofari ngapi zinahitajika, cement n.k

Mbona inafanana na zile polisi post za Lyatonga?
 
Back
Top Bottom