Ushauri wa Mahitaji kuhusu biashara ya kuchomelea (welding)

Kwenye kupima diameter (Internal/External diameter), kifaa kinachotumika kinaitwa Vernier Caliper.
Zipo za aina 2, Analogy na Digital Vernier Caliper.
Japo kwenye ufundi Welding sicho cha muhimu sana, labda Kama utakuwa unafanya Design.
Bei zake zungukia maduka makubwa ya hardware.
 
Na hizi vice za kg 7 utofauti wake na hzo vice kubwa ni upi maana kama chuma kinaweza ingia kati kati cha size yyte vice itashndwa kukikamata au kukikaza?

kazi za vice kubwa kubwa ni zipi mkuu?
Utofauti wa vice kubwa na ndogo Ni uwezo wake wa kubana (gripping Force), vice ndogo inabana kwa force ndogo.
Pia ukubwa wa work piece/material, vice kubwa ina uwezo wa kubeba/kubana mzigo mkubwa zaidi bila kufail.
kazi ya vice kubwa kubwa Ni kwa ajili ya kubana/kubeba mizigo mikubwa.
 
Asante sana kwa elimu Elon Mzebuluni Mungu akubariki sana.
Asante mkuu.
Mimi Ni mtengezaji wa mapambo kwa ajili ya uchomeleaji yaani Welding decorations, kwa ajili ya madirisha, mageti, milango, fensi, balcony, mapambo ya vitanda vya chuma, mikuki ya mageti.
Kwa Io mkuu ukipata kazi za wateja wanao hitaji mapambo hayo katika kazi zao, usisite kuniungisha.


Hizi Ni baadhi ya samples.











 
Mkuu nahitaji roller KWA ajili ya geti la gari la ukubwa wa 500cm urefu×250 cm upana, unazo?
 
Mkuu kwema? Naomba kuuliza swali.
Mimi sina utaalamu kabisa na mambo ya uchomeleaji. Ila nimepata wazo la kufungua kijiwe cha uchomeleaji. Nataka kununua vifaa vyote vya uchomeleaji halafu niajiri mafundi wa kuchomelea. Je, makubaliano ya malipo na mafundi yatakuwaje. Najua kuibiwa kupo, ila nataka kuwa na uhakika wa kuingiza hela kila siku hata mafundi wajue kila siku tunatakiwa kutoa hela kwa mmiliki wa vifaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…