Kwa wale mnaoishi maisha ya gym na diet, vip mabadiliko ya miili mnayaona?? Tunaomben ushauri hapa mazoezi yapi tufanye, diet twende nayo vip, ili kupunguza kilo maana zimeongezeka kwa kasi.. [emoji18][emoji119]
Pole sana ila bora umewai kabla haujanenepa kupitiliza.
Kwenye swala la chakula
1. acha vitu vya sukari na matumizi ya sukari kabisa
Soft drinks achana nazo, beer, juice za viwandani nk
2.Acha kula wali, ikitokea umekula wali basi kheri ule mchana na sio usiku. Kama unapenda wali basi kula brown rice
3. Acha kula vitu vya kukaanga, chemsha au choma
4. Jitahidi ule masaa mawili kabla ya kulala.
5.Kunywa maji ya kutosha.
Kwenye swala la mazoezi mwezi kabla ya kuanza gym
1.Kabla ya kuanza gym, anza kwa kutembea angalau nusu saa kila siku
2. Ruka kamba at least dakika 15 kila siku
Hii itakusaidia hata ukiwa teari kwenda gym mwili unakuwa mwepesi kidogo, na mwili unakuwa ushazoea mazoezi kwaio uta enjoy.
Faida za kwenda gym
1. Kutoa pesa inauma, ukitoa pesa yako itakua inakuuma kukosa kwenda mazoezi, kwaio kile kitendo cha kuwa na uchungu kitakusaidia usi miss mazoezi na mwishowe utaona mabadiliko
2. Gym kuna watu wengi, yani uwezi fika wenzio wote wapo busy na mazoezi wewe una chat au umelala, kwaio utaona aibu
3. Competition, utakutana na watu wanaopambana kama wewe kupungua kwaio utajikuta unataka u compete nao na hivyo utaongeza jitihada
4. Inspiration, wana gym wataku inspire ufikie lengo lako
NB: Kuona mabadiliko binafsi inachukua mpaka week 3, utaanza kujiona umekuwa mwepesi, kuna nguo zilikua hazikutoshi zinaanza kukuenea, mashavu kupungua nk
Inachukua miezi 3 watu wengine kukuona kuwa umepungua, hivyo usikate tamaa ukiona kama watu hawakusifiii