Ushauri wa mazoezi na diet

mwalimu wako na wangu nadhani ni mwalimu mmoja.
keep it going
 
safi sana
 
Hakuna zoezi linakata kitambi kama jogging.

Miezi mitatu pekee imenitosha kupunguza kitambi chote.
 
Wanasema "body bulding is journey" ili kuhakikisha una maintain uzito inahitaji muda hasa kwa wale wanene kupitiliza..lakn kuna key principle ambazo unaweza kutembea nazo ili kuhakikisha unakua na mwonekano wa kawaid a yan mediam kama wengi wanavyopenda,vyakula vya viwandan kama soda,biscut na pipi unatakiwa kuanza kupunguza taratibu.
Anza kupendelea zaid vyakula vya asili kama karanga,asali,mbogamboga matunda na kadhalika.
Anza kupunguza vyakula vya kukaangizwa kama chips,nyama,kitimoto na kadhalika.
Nafaham kuacha moja kwa moja si rahisi lakin kwa kupunguza inaweza kukusaidia pia..
Anza kupendelea kunywa maji kwa wingi hasa siku ukiwa nyumbani .
Anza kufanya Mazoez madogo madogo siku ambazo upo free hom kama vile kunyoosha kiuno,kuinamaa,kukaa,kuruka kamba,kuruka juu na push up kidgo
Penda kutembeaa kwa miguu au tumia baiskelii just kupiga round tuu siku za weekend
Jiunge n'a joging clab au kimbia ww mwenyewe pale unapopata nafasi
Punguza ngono kama kijana..utaishi maisha ya aman n'a furaha.
Asanten.
 
Hapo kwenye kuacha chips sasa[emoji36][emoji36]
 
Kwa wale mnaoishi maisha ya gym na diet, vip mabadiliko ya miili mnayaona?? Tunaomben ushauri hapa mazoezi yapi tufanye, diet twende nayo vip, ili kupunguza kilo maana zimeongezeka kwa kasi.. [emoji18][emoji119]
Pole sana ila bora umewai kabla haujanenepa kupitiliza.
Kwenye swala la chakula
1. acha vitu vya sukari na matumizi ya sukari kabisa
Soft drinks achana nazo, beer, juice za viwandani nk

2.Acha kula wali, ikitokea umekula wali basi kheri ule mchana na sio usiku. Kama unapenda wali basi kula brown rice

3. Acha kula vitu vya kukaanga, chemsha au choma
4. Jitahidi ule masaa mawili kabla ya kulala.
5.Kunywa maji ya kutosha.

Kwenye swala la mazoezi mwezi kabla ya kuanza gym
1.Kabla ya kuanza gym, anza kwa kutembea angalau nusu saa kila siku
2. Ruka kamba at least dakika 15 kila siku
Hii itakusaidia hata ukiwa teari kwenda gym mwili unakuwa mwepesi kidogo, na mwili unakuwa ushazoea mazoezi kwaio uta enjoy.

Faida za kwenda gym
1. Kutoa pesa inauma, ukitoa pesa yako itakua inakuuma kukosa kwenda mazoezi, kwaio kile kitendo cha kuwa na uchungu kitakusaidia usi miss mazoezi na mwishowe utaona mabadiliko
2. Gym kuna watu wengi, yani uwezi fika wenzio wote wapo busy na mazoezi wewe una chat au umelala, kwaio utaona aibu
3. Competition, utakutana na watu wanaopambana kama wewe kupungua kwaio utajikuta unataka u compete nao na hivyo utaongeza jitihada
4. Inspiration, wana gym wataku inspire ufikie lengo lako

NB: Kuona mabadiliko binafsi inachukua mpaka week 3, utaanza kujiona umekuwa mwepesi, kuna nguo zilikua hazikutoshi zinaanza kukuenea, mashavu kupungua nk

Inachukua miezi 3 watu wengine kukuona kuwa umepungua, hivyo usikate tamaa ukiona kama watu hawakusifiii
 
Umetoa bonge la elimu. Pongezi kwa elimu ulompatia.
Nisilibe tuu
Mazoezi ni mazuri sana ila hayapunguzi mtu haraka kama chakula hasa wanga na sukari.
Niliwahi msimamia mtu katika kupunguza mwili.yan nkawa nafanya jukumu la kumpangia na kumwandalia vyakula vya vyakula kuanzia kifungua kinywa mpaka chakula cha usiku. Ndan ya mwezi mmoja kilamtu anamwambie sasa umepungua naumependeza.
Kupungua mwili ukiamua ni rahisi ila ikiwa kama unajilazimisha utaona tabu
 
kabisa
 
Naachaje kula ugali mimi😭😭😭
 
Hapo pa kuacha sukari, inamaana hata chai hutakiwi kunywa, au inakuaje mkuu
 
Ni kweli. Mazoezi nayo wito😀😀...nikifanya leo inapita wiki sijafanya, haileti matokeo mazuri
jiwekee zawadi, tafuta kitu ambacho unakipenda alafu jiahidi kujizawadia ukikamalisha kitu ambacho ni kigumu kwako kukifanya.
 
jiwekee zawadi, tafuta kitu ambacho unakipenda alafu jiahidi kujizawadia ukikamalisha kitu ambacho ni kigumu kwako kukifanya.
Kama ninachokitaka kipo nje ya uwezo wangu inakuaje? Labda mtu aniahidi zawadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…