Naandika haya nikiwa katika Jiji la Dar es Salaam, moja ya sehemu chafu kimazingira katika nchi yetu. Najaribu kuwaza uhusiano uliopo kati ya umaskini na uchafu lakini bado sijaona sababu ya msingi ya umaskini wetu kutufanya tuishi katika mazingira machafu. Nimwaza njia zifuatazo zinaweza kutumika kuweka miji na majiji yetu katika hali ya usafi.
Moja, elimu kwa raia. Ukiona kila ukuta umeandikwa "Usikojoe Hapa", kinachokuja akilini haraka ni elimu ya watu katika mazingira husika. inakuwaje mtu mwenye upeo mzuri wa kuchanganua mambo anajisaidia kichochoroni. Elimu juu ya usafi kwa raia iwekewe mkazo kama tunavyokazia maswala mengine ya msingi kwa raia wetu.
Pili, viwanda vinavyoshiriki katika kuleta bidhaa mbali mbali kama vocha, pipi, biskuti na chupa za juice watozwe kiasi fulani ambacho kitaenda kusaidia usafi wa miji na majiji. Na katika seheu yao ya kurudisha kwa jamaa kiasi kiwekwe kwenye kununua ndoo za kutunza uchafu.
Tatu, ununuzi wa vifaa vya kukusanyia uchafu. Unatembea Posta eneo ambalo ndio limeendelea sana kwa jiji la Dar lakini hukuti ndoo ya kuweka takataka hata moja, unategemea raia watatupa wapi takataka zao. Ili kuepuka vifaa hivyo kuibiwa tunaweza kutengeneza muundo ambao utatumika tu kwa vifaa vya serikali. Hivyo mtu akikutwa nacho tunajua ameiba.
Nne, kila mwenye biashara wauza machungwa, mahindi, pipi, biskuti na kila mfanyabiashara mdogo mdogo sharti katika eneo lake la kazi awe na sehemu maalumu ya kutunza takataka zinazoletwa na wateja wake. Na pia awe na wajibu wa kwanza kusafisha eneo lote linalomzunguka katika shughuli yake. Hili lingesimamiwa vyema na watoza ushuru lingesaidia sana,hufanyi usafi hakuna kufanya biashara.
Tano, majengo yote yaliyo katikati ya jiji iwepo sheria lazima yapakwe rangi yasikae katika hali ya kuchakaa, kama ilivyo kwenye magari basi na jengo lilibabuka rangi au bati lenye kutu mjini muhusika apigwe faini.
Najua wadau wengi mnakerwa na uchafu wa miji yetu naomba tutoe maoni hapa lipi lifanyike ili kuwasaidia kimawazo wahusika maana naona kama tunafeli sana na majiji yetu yanatia aibu.