Ushauri wa Peter Manyika kwa Beno Kakolanya ni wa kinafiki

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
16,784
Reaction score
23,312
Peter Manyika golikipa wa zamani wa Yanga amekaririwa na blog ya Salehe Jembe akimshauri Beno Kakolanya arudi kumwomba msamaha mwalimu wake Zahra ili arudishwe kikosini.

Pia amegundua Benno Kakolanya amekuwa akizungukwa na watu wanaompa ushauri mbaya. Lakini Peter Manyika amesahau kuwa ni yeye aliyemwondoa mtoto wake Manyika Junior na kuvunja mkataba kwa sababu ya kutotimiziwa mahitaji yake wakati wa usajili na pia kutolipwa mishahara yake kwa wakati.

Hivi madai ya mtoto wa Manyika na Benno Kakolanya yana tofauti gani? Pia kama alimshauri mtoto wake kuvunja mkataba ina maana alikuwa anampa ushauri mbaya kama alikuwa anampa ushauri mzuri kwanini awaone watu wanaomzuka Benno wakimpa ushauri sawa na ule aliokuwa anatoa mtoto wake kuwa ni watu wabaya

Huu ni unafiki wa wazi mahaba ya timu yake ya zamani yanamfanya awe kipofu.
 
Tofauti IPO..Beno ana namba Yanga..ila Manyika Jr alikuwa anachoma mahindi Mikiani
 

Si viongozi wa Yanga walitaka kuwapatanisha Kakolanya na Zahera, kocha akakomaa na kuwatoa mbio? Kwa ufupi dogo alitaka yaishe ila Zahera aligoma katakata ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine wanaodai haki zao wasigomee mechi. Ushauri wake angeupeleka kwa Zahera kwanza
 
Simba tumsaidie kakolanya kuvunja mkataba halafu tumchukue...ni tz1 material!!
 
Tofauti IPO..Beno ana namba Yanga..ila Manyika Jr alikuwa anachoma mahindi Mikiani
Manyika Jr hakuvunja mkataba na Simba, Bali uliisha na akahamia Singida United, huko alikuwa anapata namba, tatizo likawa kupata mshahara kwa wakati, ndipo Baba yake ambaye pia Meneja wake alipomwongoza mwanae kuvunja mkataba na kuhamia timu nyingine nchini Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…