rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Peter Manyika golikipa wa zamani wa Yanga amekaririwa na blog ya Salehe Jembe akimshauri Beno Kakolanya arudi kumwomba msamaha mwalimu wake Zahra ili arudishwe kikosini.
Pia amegundua Benno Kakolanya amekuwa akizungukwa na watu wanaompa ushauri mbaya. Lakini Peter Manyika amesahau kuwa ni yeye aliyemwondoa mtoto wake Manyika Junior na kuvunja mkataba kwa sababu ya kutotimiziwa mahitaji yake wakati wa usajili na pia kutolipwa mishahara yake kwa wakati.
Hivi madai ya mtoto wa Manyika na Benno Kakolanya yana tofauti gani? Pia kama alimshauri mtoto wake kuvunja mkataba ina maana alikuwa anampa ushauri mbaya kama alikuwa anampa ushauri mzuri kwanini awaone watu wanaomzuka Benno wakimpa ushauri sawa na ule aliokuwa anatoa mtoto wake kuwa ni watu wabaya
Huu ni unafiki wa wazi mahaba ya timu yake ya zamani yanamfanya awe kipofu.