Divorce .... Divorce!!
Ni ngumu kweli kufanya. Of course tafiti nyingi hata huko marekani zinaonesha kuwa wanaoachana wengi wanaumia zaidi kisaikolojia baada ya kuachana na vile vile tafiti zinathibitisha kuwa wanawake wanaumia zaidi baada ya ndoa zao kuvunjika kuliko wanaume. Inawezekana ndo maana kina mama wanang'ang'ania zaidi.
Lakini vile vile tafiti zinathibitisha kuwa ndoa nyingi zinapovunjika; yaani wanandoa wanakuwa wamechelewa sana katika attempts za kuokoa ndoa. Yaani ndoa zinafikia kuvunjika wakati damage kwa wahusika imeshakuwa kubwa mno! Inawezekana kama wangevunja ndoa mapema madhara ya kuvunja ndoa yangekuwa madogo huko mbele. Kukaa kwenye migogoro ya ndoa kwa muda mrefu kinaumiza mno na kinaacha madhara yasiyotibika tena.
Vile vile tafiti zinathibitisha kuwa wale ambao ndoa zao zimevunjika, wanakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kushindwa kuhimili mikiki mikiki ya mahusiano yafuatayo. Yaani, ndoa yako ya kwanza ikishavunjika, uwezekano wa ndoa inayofuata kuvunjika ni mkubwa zaidi.
Sasa issue ya Boss kuwa kwa nini wanawake wanaonekana kuwa wagumu zaidi kukubali? Sina majibu! Ila mojawapo ya sababu ni Mapenzi kwa anayetaka muachane, Ugumu wa maisha au Kuwa na makosa, dini, n.k.
- Mapenzi kwa maana kuwa mume anaweza akawa hampendi mke wakati mke bado anampenda. Hapo mke atajalibu hiki na kile ili kuokoa ndoa yake na inakuwa vigumu kukimbilia talaka.
- Ugumu wa maisha - Kwa nchi zetu hizi maskini hali ya maisha ni ngumu mno na wanawake ni waathirika zaidi. Hivyo kuachana kwenye ndoa mke wakati mwingine anaona kuwa atakuwa anaukata mkono unaomlisha.
- Kuwa na makosa - Inawezekana deep inside mke anajua anamakosa katika huo mgogoro - yaani anajua amechangia sana mme wake kutaka kumtaliki na anajua talaka ikitoka makosa yake yatajulikana na jamii itamnyanyapaa.
- Dini - Nyingi haziruhusu ndoa kuvunjika. Na wanawake wengi tunajua ndo wanaojaa kwenye makanisa (ndo yanazuia ndoa kuvunjika). Hivyo mwanamke atakuwa akijaribu kuomba na kusali akiamini ndoa yake itaokoka.
Baada ya hayo msimamo wangu ni kuwa ni afadhali hali ikiwa mbaya mtengane na mkikaa mbali kwa kitambo bila kuhitajiana ni vizuri kuachana kabisa tena mapema iwezekanavyo.
Mkiachana bila kuumizana sana na maugomvi ya muda mrefu, uwezekano wa kurudiana ni mkubwa. Mkirudiana baada ya kutengana au kuachana kabisa mnaelewana vizuri zaidi na mna chance ya kudumu kuliko ilivyokuwa mwanzoni.
Mimi mwenyewe kuna wakati nili "struggle" sana kumconvince wife wangu tutengane ili tujihoji tukiwa separate; lakini ilikuwa impossible yeye kukubali kitu hicho. OK, we survived the tsunami. Lakini bado naamini kuwa kuachana mapema ni bora kuliko kusubiri mpaka ugomvi uwe mkubwa kupindukia!!