Ushauri wa talaka kwa wanawake ............

inawezekana wanawake wanaopigania haki za wanawake
hawajaona jinsi lugha inavyowarudisha nyuma,
misamiati ya kuolewa na kuachwa inawaathiri zaidi kuliko tunavyofikiri...

Kubadili lugha ni ngumu mno japo kuwa watu wanajaribu.Siku hizi kuna matumizi makubwa zaidi ya 'kuoana' au 'kutalikiana' lakini matumizi yake yanabaki ni panapozungumzwa kiujumla tu. Linapokuja suala la mmoja mmoja basi mwanamke hawezi kusema 'nimemuoa' kwa vile inaleta picha hasi kwa mwanamme

Utasikia "Nae yule kaoa au kaolewa?" ikimaanisha kuwa jamii imegawa majukumu ya muoaji na muiolewaji, na kabla hatujabadili hilo sidhani kama tutaweza kubadili maneno
 

mimi kinachonishangaza ni woga wa hata kujadili....
yaani hapo nabaki mdomo wazi....kujadili tu woga
je kutenda?????
 
mimi kinachonishangaza ni woga wa hata kujadili....
yaani hapo nabaki mdomo wazi....kujadili tu woga
je kutenda?????

Hahah Boss hujui kuwa ' The guilty are always afraid'?

Sasa mtu anaogopa asije kujadili akajikuta kuwa yeye ni miongoni mwa hao wanaoendelea kuchezea kipondo na hajatoa/dai talaka kwa hofu zisizokuwepo tu
 
I support Talaka vizuri sana pale mambo yanaposhindikana maana uvumilivu una kikomo chake. Maisha yenyewe tunaishi mara moja,sasa kwanini niwe nang'ang'ania kukaa na mtu ambaye tumeshashindwana?!!

Suala la watoto- Ni kweli kuwapa watoto kipaumbele ni jambo muhimu sana lakini hii haitoweza kunifanya nibaki kwenye ndoa kisa watoto. Mtazamo wangu ni kuwa unaweza kuwalea watoto kwa situation mbali mbali na wakawa na maisha tofauti na mazuri baadae. Wangapi wamepoteza wazazi wakiwa wachanga (yaani kufariki) au kulelewa na bibi/babu nk?! halafu mbeleni wanaweza kuwa na maisha ya furaha na mafanikio ukiacha walivyolelewa. Japo sijakataa, wazazi wakiwalea ni vyema kabisa ila siyo kutumia kigezo cha watoto.

Kuogopa jamii- Katika kitu ambacho hakiniumizi kichwa na ni kufanya maamuzi yangu bila kujali jamii inahisi nini. Kama ninaeishi maisha ya ndoa ni mimi halafu napatwa na misukosuko isiyosuluhishika basi talaka tutapeana vizuri. Siogopi ndugu, familia au hata jamaa.

Muhimu- Watu kuelewa talaka ni jambo gumu sana na linaitaji muda wa kufikiria na kutuliza kichwa maana mtu mwingine unaweza kchanganyikiwa. Ukiwa unafikia hatua hii, unahitaji muda binafsi na mpe mwenzio muda maana haimaanishi anakuzuia. Nadhani hili ndilo linachanganya wanaume wengi kuona wanawake hawataki talaka, tulia na mtamalizana vizuri. Hamuwezi kuwa mlikutana kwa amani, mkatongozana, kuwa wapenzi hatimae wachumba na wanandoa halafu utegemee talaka itelekezwe ndani ya siku moja au wiki. Kuanza na kumalizana kunachukua muda.
 
Hahah Boss hujui kuwa ' The guilty are always afraid'?

Sasa mtu anaogopa asije kujadili akajikuta kuwa yeye ni miongoni mwa hao wanaoendelea kuchezea kipondo na hajatoa/dai talaka kwa hofu zisizokuwepo tu

sasa hivi kuwa na internet na kuendesha magari
na kusema upo 'karne ya ishirini na moja' kuna maana gani?????
kama hata kujadli jambo while anonymous..huwezi????
tena linakuhusu..
 
sasa hivi kuwa na internet na kuendesha magari
na kusema upo 'karne ya ishirini na moja' kuna maana gani?????
kama hata kujadli jambo while anonymous..huwezi????
tena linakuhusu..

Ttaizo ni kuwa kwa wengi hapa JF si anonymous

Watu wameunda urafiki nje ya screen na kuelezana habari zao za ndani (Labda)..

Sasa hapa utasemaje? Ukisema kitu unaona kinamhusu Member A au ukisema vile unajua Member B anajua kama hilo ni tofauti na reality ya msemaji?
 
kama kuna ushauri mbovu ambao nimeshawahi kuona duniani ni eti vumilia tu yataisha,mungu atatenda miujiza,nani kasema,hakuna kitu kama hicho,hakuna mtu atakaye weza kuvumilia na kuwa mwaminifu kwa mwenzake kama mapenzi hakuna,madhara yake ni uoga wa kijinga kuwa mmeacha wakati kila mtu anatafuta furahaa nje kwa jinsi anayo jua,mwisho wa siku tunazika wote na kuacha yatima,me i thnk ule msemo wa kanisani eti mpka kifo kiwatenganishe ufe kabisa,mapenzi yakiisha kila mtu asepe zake,ni mtizamo tu lakini
 
na wewe hata kujadili unaogopa?
kweli kazi mnayo......

I support divorce 101%.....kwanza kwa ajili ya kuwalinda/heshima kwa wanangu...pili kwa ajili yangu binafc, wazee walitengana but 2lishukuru kwa huo mtengano kuliko 2liyokuwa tunayaona yakiendelea hapo nyumbani, mzee we2 alikuwa ni kiboko, kwa upande wa vimada/kipigo/ma2nzo kwe2 ni kasheshe, mama aliamua ku2somba na kuanza maisha mapya, mama wa watu alitulea kwa bidii/jitihada zote mpaka tulipofikia na mzee ndio alitusahau kabisa kabisa, majuto uzeeni mwenzie akila kilaini yeye akihangaika sema 2 ndio mzee wako utafanyaje......2liishi maisha mazuri/amani na mama kuliko tulivyokuwa pa1 na mzee.....siishabikii but ina umuhimu wake sana 2.
 


ambacho wanawake wengi hawajui ni kuwa
wanaume hatuwaheshimu wanawake wanaovumilia upuuzi wetu...
tunawaheshimu wale wenye guts za kusema 'tuachane'.....
 
unaona sasa The Boss,mi ndo mana uzi huu nimeuruka futi mia!
yaani we acha tu, ingekuwa tunaomba talaka kila kosa, ndoa nyingi kwa sasa zingekuwa chali, ukizingatia nyie wenyewe mlishasemaga hapa kuwa mwanaume ni mwanaume na mke ni mke, kwa hiyo mwanamme ana uwezo wa kutoka nje ya ndoa na kuendelea na mkewe, sasa kosa kama hilo na ambalo ndio tunalichukulia ni kubwa sana inakuwaje hapo? wakati mwingine kumbe huwa mnatu miss lead tu eeeeeee
 
mbona nahisi kama uvumilivu wangu ulizaa matunda
au hiyo pia haijalishi

kama ni ile kesi yako yenye 'mazingara ndani yake'....
hiyo ni kesi nyingine......

mimi nazungumzia wale wanaosimangwa,kutukanwa mbele ya watoto,
kupigwa mbele ya watoto na still 'wanavumilia'.....
 

kila kitu ni wewe na principle zako
kama kwako ku cheat sio ishu,ni poa tu...
but mimi nazungumzia zaidi ndoa ambayo
'imeshakufa' lakini mwanamke hataki talaka
sisemi makosa yasisamehewe....nasema ni kuwa
umechoka na ndoa lakini unavumilia...why?
 
kama ni ile kesi yako yenye 'mazingara ndani yake'....
hiyo ni kesi nyingine......

mimi nazungumzia wale wanaosimangwa,kutukanwa mbele ya watoto,
kupigwa mbele ya watoto na still 'wanavumilia'.....
ooooooh hapo nimekuelewa, kupigwa mateke na kubakwa au sio
 
ooooooh hapo nimekuelewa, kupigwa mateke na kubakwa au sio

wanabakwa na kutukanwa daily....
au mwanaume anahamia kwa kimada
na kukaa miezi auu mwaka..
na wewe unavumilia eti atarudi tu....
ujinga huo ndo nauzungumzia hapa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…