Ushauri: Wabunge bila kumuondoa Spika/Naibu Spika hamtaheshimika kwa wananchi na hata Rais

Ushauri: Wabunge bila kumuondoa Spika/Naibu Spika hamtaheshimika kwa wananchi na hata Rais

Paf

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
1,703
Reaction score
3,307
Waheshimiwa wabunge mmekuwa mkiburuzwa na kiti cha Spika bila kujua yeye hana chakupoteza 2025. Kwani ni automatic ni mstaafu.

Hivyo anajikomba kwa Rais kuwa mstaafu mtarajiwa mwema huku akiwaharibia ninyi.

Ushauri: Pigeni kura za siri zakutokuwa na Imani na kiti cha Spika/Naibu wake ili Bunge liwe na makali ya kibunge.

Kiti cha Spika kimekuwa kinaongaza kwa ubabe kwa matakwa yake, ipo mifano mingi ambayo inashusha hadhi ya Bunge na Serikali.

Mkifanya hivyo mtakuwa mmefanya jambo la historia kwa manufaa ya nchi.
NB

Angalieni udhaifu wa mawaziri hawa ambao hawajawa msaada ndani ya Bunge na nje ya Bunge.

1. Sheria na Katiba
2. Mwanasheria Mkuu
3. Wizara ya Fedha
4. Wizara ya Afya

Hawa wamekuwa sehemu ya upepo unaelekea wapi wa Rais, ndio maana mitaani ni malalamiko kila siku.

Kazi kwenu wabunge huko majimbo kusikiliza maoni ya wananchi na wanachama ili muwe na msimamo mmoja mnaporudi Bungeni.
 
Shida iliyokuwa dhahiri shahiri ni pale chaguzi zile za serikali za mitaa na ule mkuu utaratibu wake ulipoingiliwa kisiasa na kupelekea kupata matokeo yasio sahihi na mwisho watu wasio sahihi.
 
Wabunge gani unaowapa huu ushauri?

Hawa ambao hawakatwi kodi kwenye mishahara yao?
 
Ni bora kama shida ingekuwa hapo tu, licha ya Kinga za kutoshitakiwa za kujitengenezea, hasara na uharibifu kwa taifa, zaidi kutokana na wawili hao, ingekuwa kila Mtanzania angeweza kuipima, wote wangezirai kwanza, na tafakari ingeanza pindi wakizinduka.
 
Let's be Realistic.

Wamuondoe Spika ambaye amehakikisha / anahakikisha usiku na mchana hii keki ya Taifa wanaila vilivyo?
 
Hao wabunge wangekuwa wameingia bungeni kwa ridhaa ya wananchi sawa, lakini kwa namna walivyoingia hawana uwezo wa kupinga lolote. Hapa ndio linapokuja suala la uhalali wa madaraka.
 
Waheshimiwa wabunge mmekuwa mkiburuzwa na kiti cha Spika bila kujua yeye hana chakupoteza 2025.kwani ni automatic ni mstaafu. Hivyo anajikomba kwa Rais kuwa mstaafu mtarajiwa mwema huku akiwaharibia ninyi.
USIWAPANGIE WABUNGE WANA AKILI ZAO.
 
Sauti yenu ni sauti ya Watanzania.Mna nguvu kwenye chama kuliko Mwenyekiti Taifa.

Bunge limejaa vijana ambao hawajawa msaada wawapo Bungeni,wanamezwa na kiti cha Spika,hali iliyopelekea wananchi kulichukia Bunge.

Kumbuka Mh Rais alishasema Bunge halina afya,wanademka.Msaidieni kwa kwa kuagiza kamati za CCM na wabunge wote kuwaondoa kwenye kiti.

Wabunge kwenye nia yakumkosoa Spika anawapeleka kwenye kamati nakuua hoja yenye ukweli wakujenga nchi.

UVCCM Shinyanga mlionyesha njia kwenye TOZO,mmesaidia sauti kusikika kwa haraka,msisubiri kama Diallo mambo yaharibike.Mkipaza sauti hata makongamano ya kudai katiba mpya yatakuwa hayana nguvu.

NGUVU YENU NI SILAHA KWA WATANZANIA WOTE.
 
Sauti yenu ni sauti ya Watanzania.Mna nguvu kwenye chama kuliko Mwenyekiti Taifa.

Bunge limejaa vijana ambao hawajawa msaada wawapo Bungeni,wanamezwa na kiti cha Spika,hali iliyopelekea wananchi kulichukia Bunge....

NGUVU YENU NI SILAHA KWA WATANZANIA WOTE.
 
Attachments

  • 2850007_220078589_1690389091165713_5262137292318157038_n.mp4
    2.2 MB
Sauti yenu ni sauti ya Watanzania.Mna nguvu kwenye chama kuliko Mwenyekiti Taifa.

Bunge limejaa vijana ambao hawajawa msaada wawapo Bungeni,wanamezwa na kiti cha Spika,hali iliyopelekea wananchi kulichukia Bunge....
Wanasema samaki mkunje angali mbichi,kushindwa kufanya hivyo mwisho utamvunja,sasa hao ndio wakuona na kumkunja samaki akiwa mbichi,?

Kama kwao usiku wanalazimisha uitwe mchana wataweze kuona hayo?Wanasema wanaielekeza sirikali kupitia upya tozo, sasa Mimi nawauliza je nilini wata muelekeza sirikali kufuata sheria na Katiba kwa mujibu sheria zilizopo?
 
Sauti yenu ni sauti ya Watanzania.Mna nguvu kwenye chama kuliko Mwenyekiti Taifa.

Bunge limejaa vijana ambao hawajawa msaada wawapo Bungeni,wanamezwa na kiti cha Spika,hali iliyopelekea wananchi kulichukia Bunge....
UVccm wa nchi gani hao? Hawa akina K?
 
hayo ni majungu tu wanatatizo gani hao
Msipopitisha bajeti Bunge Rais anavunja Bunge.Hayo ni majungu?
Huwezi kuona umuhimu wa Bunge kujitegemea siyo lazima uchangie
 
Sauti yenu ni sauti ya Watanzania.Mna nguvu kwenye chama kuliko Mwenyekiti Taifa.

Bunge limejaa vijana ambao hawajawa msaada wawapo Bungeni,wanamezwa na kiti cha Spika,hali iliyopelekea wananchi kulichukia Bunge...
Unawaonea hao vijana, jukumu lao kubwa walilopewa ni kumjibu (tena kwa kashfa) yeyote yule atakayetoa/mwenye mawazo tofauti na viongozi wa serikali. kama wanavyofanya kwa wapinzani na pia walivyofanya kwa Diallo na Mh. Mtaka. huwa hawataki mawazo mbadala.
 
Back
Top Bottom