Ushauri: Wabunge wamchague Spika asiyetokana na chama

Sio kwa bunge hili Mkuu lazima wampitishe kijani mwenzao
 
Sasa si mpaka hao wenye wagombea wenye sifa wajitokeze kwanza?
 
Ndiyo Mtanzania yoyote mwenye sifa ya kuwa Mbunge (umri, uraia, elimu) anaruhusiwa kugombea Uspika bila Chama na Wabunge wote (hata wa CCM) watamchagia
Kifungu chakl 84(1) kimalizie panaposema au mwenye sifa za kuwa Mbunge
Kifungu 84(9)
Mtu yeyote ambaye sii Mbunge atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa kabla ya kuanzja kutekeleza ataapisha katika Bunge kiapo Cha uaminufu (maana yangu NI kabla ya Cha Uspika
fomu zinapatikana kwa Katibu Bunge hata CCM watapewa / kununua tafsiri yangu) ninayo majina ya wagombea binafsi waliopambana na Maspika
Sasa mleta mada anamaanisha spika asie na chama ndio apigiwe kura ndo maana nikamuuliza hiyo katiba inasema hivo???spika asie na chama???rejea uzi wake hapo juu soma vizuri utamuelewa
 
Katiba inaruhusu?
 

Jaribu kuwa practical mkuu. Duniani kote Siasa ziko hivyo. Chama kinajilinda. Sasa wewe utoke nje ya chama nani atakuchagua. Hao wabunge wako pale na Ni wanasiasa.
 
Lakini hiyo katiba haijawahi fuatwa tangu tupate uhuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM itaweka mapandikizi tupu kama ilivyo mahakamani, tume ya uchaguzi na polisi
CCM kwa sasa ni laana kwa nchi. Ipo zaidi kwaajili ya uharibifu kuliko mema.

CCM ndiyo kikwazo kikubwa kwa mifumo bora uongozi nchini. Bila ya CCM kuondoka madarakani, kamwe nchi hii hatutakuja kuwa na mifumo bora ya kiutawala. Hakuna mahali CCM inafanya kwa dhamira njema zaidi ya kuhakijisha inabakia madarakani kwa njia zozote zile hata kama ni za kishetani.

Inaangilia mifumo ya kimahakama, bungeni, jeshini, polisi, TISS, ofisi ya CCG, DPP - kila mahali inachafua.
 
Kumbukeni Bunge letu limejaa wabunge wa hovyo wasiojali maslahi ya nchi, wao ni CCM tu
 
SPIKA LAZIMA ADHAMINIWE NA CHAMA CHA SIASA ILA ANAWEZA ASIWEZE MBUNGE. HAKUNA MGOMBEA BINAFS KWENYE USPIKA TUSIPINDISHE SHERIA.
 
Wampe Wilbroad Slaa
 
Ni vigumu kumpata spika asiyetokana na chama! hii ni kwa sababu mgombea nafasi ya u-spika ni lazima awe na sifa za kumwezesha kuwamgombea ubunge! ambapo mojawapo ya sifa hizo ni lazima atokane na chama cha siasa, ila kwa kutofuata katiba wala mifumo rasmi hiyo itawezekana!! Nakumbuka kuwahi kuwepo nafasi ya Naibu Waziri Mkuu kama sijakosea!!!Ni ile nafasi ya mzee wa TLP
 
Hiyo (b) ina maana haipewi umuhimu? Binafsi bado nasimamia lazima atokane na chama cha siasa, rejea pia katiba pendekezwa 125(1)c
 
Sifa mojawapo ya Spika ni kuwa na sifa za kuwa mbunge. Sifa za kuwa mbunge ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa kama Katiba ilivyoainishwa hapa chini:

67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo- (a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza; (b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa; (c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Kwa sababu hiyo, hauwezi kugombea uspika bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa na kupendekezwa na chama cha siasa. Hamna cha mgombea huru kwenye hili.

Amandla...
 
Jamaa ni waharibifu sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…