Ushauri: Wafanyabiashara, muda muafaka wa kuanzisha Bank yenu

mbota

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
1,054
Reaction score
585
Salaam wapendwa.

Wafanyabiashara wa Tanzania nina ushauri kwenu baada ya kusikia malalamiko mengi kuhusiana na maswala ya mikopo, au huduma zitolewazo. Kwanza ninaamini wafanya biashara ndio wanaosaidia sana mzunguko wa fedha katika eneo fulani. Pili wafanyabiashara ndio wanao chukua mikopo mikubwa kulinganisha mfano wafanyakazi

Hivyo ninaa mini kwamba wafanya biashara wakiamua kuanzisha Bank yao inawezekana kwa maana wafanya biashara ni wengi na wengi wao wana mitaji ya kutosha kikubwa ni usimamizi mathubuti.

Faida ya kuwa na Bank ya wafanya biashara ni kwamba wafanyabiashara watapata huduma kwa wakati na si kama ilivyo sasa.

Kama Walimu waliweza naamini Wafanyabiashara pia wanaweza.
 
Mkuu hilo ni wazo zuri sana, naamini kama likifanyiwa kazi hakuna bank ambayo ingekuwa mbele kama hii. Huenda hata zile ambazo tayari zipo zingeyumba kiasi, imagine ni wafanyabiashara wangapi wanaotumia bank na hizo hela zinaenda kwa wengine. Kama kukawa na watu smart hili ni wazo zuri na lenye maisha ya kweli.
 
Kweli kabisa JUKUMU yani Nina uhakika lazima bank nyingine Zita weweseka Kama bank ya wafanya biashara itaanza
 
Last edited by a moderator:
Salaam wapendwa.

Wafanyabiashara wa Tanzania nina ushauri kwenu baada ya kusikia malalamiko mengi kuhusiana na maswala ya mikopo, au huduma zitolewazo. Kwanza ninaamini wafanya biashara ndio wanaosaidia sana mzunguko wa fedha katika eneo fulani. Pili wafanyabiashara ndio wanao chukua mikopo mikubwa kulinganisha mfano wafanyakazi

Hivyo ninaa mini kwamba wafanya biashara wakiamua kuanzisha Bank yao inawezekana kwa maana wafanya biashara ni wengi na wengi wao wana mitaji ya kutosha kikubwa ni usimamizi mathubuti.

Faida ya kuwa na Bank ya wafanya biashara ni kwamba wafanyabiashara watapata huduma kwa wakati na si kama ilivyo sasa.

Kama Walimu waliweza naamini Wafanyabiashara pia wanaweza.
Brilliant idea!
 
Tena waanzishe bank na waweke matawi makubwa kule wanapofanya shughuli zao mfano kariakoo, posta etc
 
kwa nchi hii hili halitawezekana, maana viongozi wamezoea kupokea rushwa kwenye haya mabenki yaliyopo, kuruhusu hili itakuwa kujifungia wenyewe mianya ya rushwa.
 
Mbota wazo lako zuri sana, kama utakuwa na nafasi jaribu kutafuta namba ya Minja yule mwenyekiti wao. then mpe wazo hili. Ninaamini laweza fanyiwa kazi
 
Hivi bank nayo pia si biashara au?

Ni biashara lakini wanaofanya hii biashara bado hawawajali wafanya biashara wa chini, wa Kati na wale wakubwa na ndio dhamira Yangu ya kushauri waanzishe yao
 
Mbota wazo lako zuri sana, kama utakuwa na nafasi jaribu kutafuta namba ya Minja yule mwenyekiti wao. then mpe wazo hili. Ninaamini laweza fanyiwa kazi

Nalifuatilia MKUU nitaleta mrejesho
 
Wakuu habari zenu nawashukuru sana kwa michango yenu kuhusu hili wazo
Jana kwenye taarifa ya habari niliona jumuiya ya wafanya biashara pamoja na wenye viwanda wameadhimia kuanziasha bank yao na sababu kubwa waliyotoa ni kwamba bank zilizopo siyo rafiki kwao JUKUMU mwasu geofreyngaga Bulldog jamiimemba ssafari
 
Wametoa wazo na wanaweza anzisha ila lazima itapenyezwa fitna huko mpaka wakome, au wawe tayari kuikopesha serikali mikopo isiyolipwa, na kufadhili kampeni ya chama tawala hapo watabaki salama, wakileta ubishi watapigwa tu, maana hamna jinsi lazima ipotee.
 
Huo ndio wasiwasi wangu mkubwa tangu mwanzo. Sbb kama ikifanikiwa kuanzishwa na ikawa na mashart yasiyo magumu sana watawapata wateja wengi.

Lkn ishu nyingine ni kweli wataweka mashart rahis? Maana kuna miradi uwa inaanzishwa kwaajili ya watu wa kawaida lkn kiukweli ukifuatilia na fix tupu.
 
Bonge la idea ila sijui kama kibongo bongo watafanikiwa.
 
Salaam wapendwa.

Wafanyabiashara wa Tanzania nina ushauri kwenu baada ya kusikia malalamiko mengi kuhusiana na maswala ya mikopo, au huduma zitolewazo. Kwanza ninaamini wafanya biashara ndio wanaosaidia sana mzunguko wa fedha katika eneo fulani. Pili wafanyabiashara ndio wanao chukua mikopo mikubwa kulinganisha mfano wafanyakazi

Hivyo ninaa mini kwamba wafanya biashara wakiamua kuanzisha Bank yao inawezekana kwa maana wafanya biashara ni wengi na wengi wao wana mitaji ya kutosha kikubwa ni usimamizi mathubuti.

Faida ya kuwa na Bank ya wafanya biashara ni kwamba wafanyabiashara watapata huduma kwa wakati na si kama ilivyo sasa.

Kama Walimu waliweza naamini Wafanyabiashara pia wanaweza.

Bank ya walimu sio ya walimu kama ulikua hujui,wana hisa chache tu...wafanyabiashara wakifungua benk yao haitokua inafanya kazi kibiashara itakua kama charity na mwishowe itakufa kwa maana mngine mganga hajigangi.
 
Back
Top Bottom