Ushauri wako muhimu: Soko la biashara ya mahindi

Ushauri wako muhimu: Soko la biashara ya mahindi

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
7,621
Reaction score
12,505
Wakuu naomba ushauri wenu,

Kwasasa nipo Singida na kuna mahindi mengi sana huku debe hadi sh 4000.

Binafsi nina mtaji wa kama milioni 6 hivi na ninataka kuifanya biashara hii, Tatizo langu ni namna soko lake lilivyo Dar maana nataka kuyanunua niyalete Dar.

Kwa wenye ujuzi na hili soko lake likoje maana inaonekana watu wengi wanapata shida wanapokuja na biashara kuuza Dar ama kwa kutapeliwa na madalali au kubamizwa bei.

Naomba mawazo yenu.
 
We nunua,koboa,saga pack kwenye viroba vya kg 25,uza kwenye maduka ya kuuza bidhaa ,maduka ya wholesale,uza mwanza,kahama,ama hata dar,
 
Mi nakushauri nunua kwa wingi kama una eneo Zuri la kuyahifadhi afu badae yapeleke Dar mana mwaka huu mahindi dili sana mi mwenyewe nayatafuta mana nililima kwa kuchelewa kidogo na mambo yameenda ndivyo sivyo na watu wengi sana safari hi hawajapata mahindi kama walivyotarajia tokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mbolea sijui ilikuwa out dated mana duuh!
 
Kama unahitaji mahindi ya kutosha Ni PM please. kama uko serious na biashara kuna sehemu mahindi yapo ya kutosha wanunuzi hakuna.
 
Nunua weka dawa vizuri hifadhi mwezi wa 12 utauza debe kwa zaidi ya elf kumi
 
Kama unahitaji mahindi ya kutosha Ni PM please. kama uko serious na biashara kuna sehemu mahindi yapo ya kutosha wanunuzi hakuna.

Mkuu kuna tabu gani kama ukieleza hapa wapi yalipo hayo mahindi mengi na bei yake ikoje kuliko watu wote tukufuate PM?

Ni ushauri tu.
 
Mkuu kuna tabu gani kama ukieleza hapa wapi yalipo hayo mahindi mengi na bei yake ikoje kuliko watu wote tukufuate PM?

Ni ushauri tu.
nimesema kama upo serious ni PM. We inaonekana hauko serious wenzio wameshaniPM Ktambo
 
Back
Top Bottom