Ushauri wakuu, nina mpango wa kununua gari la maji taka.

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
1,718
Reaction score
461
Kama nilivyoanza hapo juu. Wilayani kwetu kuna mahitaji makubwa ya gari la maji taka na kwa muda mrefu tumetumia gari la Halmashuri ku- discharge maji taka kutoka katika vyoo vyetu hapa wilayani.

Gari la halmashauri halitoshi kutokana na urasimu uliopo kulipata na hatimaye utiririshaji wa maji hayo machafu hasa wakati wa usiku umekua kwa kasi sana. Nimewasiliana na wadau mbalimbali na tumekubaliana tununue gari la maji machafu walau lenye uwezo wa "kunyonya" lita elfu saba hivi za maji machafu kwa mara moja.

Nakuja kwenu kuomba ushauri wa gari lipi linafaa- specifications kwa maana hiyo na bei zake. Shukrani mbele.
 
Lita Elfu saba (7000) ni ndogo sana mkuu kwa maji taka!

Specifications ambazo naona ni muhimu kwa uzoefu wangu ni upate gari iko na tank Tilted End! Sewer disposal Arm, na kwa miundo mbinu tuliyo nayo haswa huko wilayani unakosema unahitaji Sucking Horse yenye urefu wakutosha.

Kwa ushauri tu avoid Hydraulic Elevated Tanks, Kumbuka hizi gari ni specified kwa kazi moja tu. Fanya utafiti wa kina wa soko lilopo na ikiwezekana kua na secured contracts ili kukaa mbali na upinzani wa Gari la halmashauri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…