Salaam kwa wana jf wote,Licha ya kupitia nyuzi mbalimbali za uanzishaji wa kampuni nimeambulia kuelewa hatua za kufuata na nn kufanya kupata kampuni yako.
Ningependa kujua yafuatayo.
Ningependa kujua yafuatayo.
- Aina ya kampuni ni kampuni binafsi yani mm ndiye mkurugenzi mtarajiwa,Hakuna hisa nitaanza mwenyewe na wasaidizo kadhaa itapokuwa kubwa mungu akijalia nitakaribisha hisa.Je nitahitaji kuorodhesha shughuli zote za kampuni yangu katika usaji?
- Vipi kama kampuni yangu ikijihusisha na shughuli ambayo sijaibainisha itachukuliwa hatua gani?sina lengo hili ila napenda kujua ili ikitokea waajiliwa wangu wamehusika nijue nini kinafuata.
- Ili kampuni ifanye multifunction mfano itoe huduma za civil engnearing pia iwe na maduka mikoa tofauti yasiyohusu civil work nitahitaji usajili kila mahali napofungua shop au naweza kutumia taarifa zile za kampuni kulipa kodi kila napofungua office(jiji au halmashauri)
- Naweza kuwa na kampuni inayofanya kazi idara tofauti mfano usafirishaji na ujenzi ikatumia jina moja nililopendekezeza Brela.