Ni ushauri tu kwa akina dada:
Leo nikiwa njiani kuelekea kwenye deiwaka kulitokea jambo ambalo kidogo ni la kusikitisha.
Akiwa kwenye daladala ambayo ilijaza kupita kiasi dada mmoja alianguka ghafla ndani ya gari hiyo. Wakati huo daladala hiyo ilikuwa imesimama kwenye foleni. Basi konda pamoja na abiria wengine waliokuwemo humo wakamsaidia kumtoa dada huyo na kumlaza pembezoni mwa barabara.
Kimavazi, dada yule alikuwa amevaa kitopu kifupi kinachobana sana pamoja na kimini.
Kutokana na tukio lenyewe lilivyotokea wakati wa kumbeba kwa kweli ilikuwa kama vile yuko mtupu (try to imagine). Basi watu waliokuwa karibu ilibidi kila mtu aanze kusema lake (hasa kuhusiana na mavazi). Wengi walilaumu kuwa akina dada wa siku hizi wanavaa nguo zinazowashika mwili lakini kwa nini wanashindwa kuweka japo kaupande kamoja ka kanga ili kiwasetiri pindi watakapopata emergence. Walikuwepo pia akina mama ambao nao walishiriki katika lawama hizo dhidi ya "mabinti" zao.
Wakati huo mimi pia nilikuwa karibu na tukio. Dada yule ilikuwa kama vile hapumui. Basi nikajaribu kuwashauri wale watu ambao walikuwa wamejikita zaidi katika kulaumu kwamba kwa wakati huo lawama haikuwa kitu cha muhimu. Badala yake tujikite katika kuhakikisha kuwa tunaokoa maisha ya binti yule huku tukihakikisha kuwa tunamsetiri utu wake. Kitu cha kwanza nilimuomba mama mmoja ambaye alikuwa amejifunga kanga atuazime kanga moja tumsetiri. Mama alikubali.
Wakati huo dada mmoja alikuwa akimpepea kwa kitambaa chepesi. Mimi niligundua kuwa hiyo isingesaidia kitu kama nitakavyoeleza hapa chini.
Kwa kuwa dada yule ali-faint katika gari ambayo ilikuwa imejaa pomoni ni dhahiri kuwa alikosa oxygen ya kutosha hivyo moyo wake kushindwa kufanya kazi sawasawa na kupelekea ubongo kukosa oxygen ya kutosha. Kitabibu, inasadikika kuwa ubongo ukikosa oxygen ya kutosha mtu anaweza akapoteza maisha ndani ya dakika 5.
Kwa kuwa mimi nina idea ya huduma ya kwanza nikaona si vibaya nikampatia yule dada huduma ya kwanza kwa kadri ninavyoweza. Kitu cha kwanza nilijitambulisha kwa watu ambao sasa walikuwa wamejaa kumzunguka yule dada bila msaada wowote na kuwaeleza kuwa ninayo mafunzo ya huduma ya kwanza.
Baada ya hapo nikamfanyia kitu kinaitwa Cardio-Pulmonary Rescusitation (CPR) kwa ajili ya kuustua moyo wake na kumwongezea oxygen. Wakati huo nilimuomba jamaa mmoja aende kutoa taarifa kwa Traffic Police ambao walikuwa upande wa pili wa barabara wakiangalia usalama wa magari. Nilimpatia jamaa mwingine achukue simu ya yule dada na ajaribu ku-search namba za jamaa zake wa karibu na kuwataarifu juu ya mkasa huo.
Mimi niliendelea na CPR hadi nilipohakikisha kuwa yule dada amepata nafuu nikamweka kwenye "Recovery Position" halafu nikamkabidhisha kwa akina mama wawili ambao walikuwepo eneo la tukio na walikuwa wakitoa msaada wa hapa na pale then na mimi nikawahi kwenye "kijiwe changu cha kuponda kokoto".
Nikiwa njiani nilijaribu kutafakari mambo mengi sana kichwani lakini kikubwa ambacho niliona si vibaya nikawashauri akina dada:
Jamani, pamoja na kupiga mapigo makali ya viwalo si vibaya kwenye hayo mapochi yenu mkaweka japo kaupande ka kanga. Huwezi jua njiani!
Note: Kisa hiki kimetokea kweli leo asubuhi kama nilivyokielezea.