Ushauri: Wanawake jengeni utamaduni wa kutembea na japo kanga moja kwenye pochi zenu.

Daaah
Sikutegemea kuona comment ya hivi, tena ya mwanamke :shock:

Wakati mwingine unaweza kudhani watu wanatumia mbinu ya kujifanya wajinga ili kujipatia umaarufu humu, lakini ndo tunawaona wajinga kweli hivyo.
 
Asante kwa ushauri, kanga ingemsaidiaje na hana fahamu, ingejitoa kwenye begi au. Mimi nasema waache kuiga mila si zao, wavae mavazi ya heshim full stop.
 
hongera kwa moyo huo lakini hata angekuwa na kanga asingeweza kujisetiri mwenyewe
 
hongera kwa moyo huo lakini hata angekuwa na kanga asingeweza kujisetiri mwenyewe
Sasa hapo ilitakiwa itumike tu busara ya walokuwapo hapo, mbona simu waliitoa ili waqaailiane na jamaa zake?
Hebu assume labda angekufa, si wangepekua tu mkopa walau kupata vitambulisho?
Hapakuwa na ugumu hapo, labda kama walifungua na wakaikosa.
 

Big Up Mkuu. Acha kuponda kokoto, tafuta kibarua kingine kizuri.
 
Umenikumbusha mbali , kuna siku tulienda kumwona jamaa mahabusu sasa tuliongozana na mdada mmoja kapiga trousers ya jeans , wakati tumeruhusiwa kwenda kumuona ghafla askari wa kike akamwita yule dada na kumwambia ajifunge kanga maana kule mahabusu ni kwa wanaume. Bahati nzuri yule dada alichukua kanga nyumbani kwake na kuiweka kwenye pakacha lakeh ivyo ilimsaidia wakati ule. Ni muhimu kuwa na kanga ama kitenge kwa akina sisters.
 
Hongera sana mkuu, Mungu akubariki sana kwa kujitolea.
Pia nahisi wamakusikia hao wasiotembea na kanga wala mitandio.
 
wakati mwingine unaweza kudhani watu wanatumia mbinu ya kujifanya wajinga ili kujipatia umaarufu humu, lakini ndo tunawaona wajinga kweli hivyo.
mkuu mimi siwezi kujitafutia umaarufu jf ror what? Nadhani kwa commet yako hii wewe ndo unaonekana mjinga zaidi
kama ni lazima mwanamke atembe na kanga ingekuwa imewekwa iyo sheria kwenye huduma ya kwanza
mimi kwangu sioni kama ni muhimu wala sitokaa nione ni muhimu kamwe,kuna njia nyingi za kukabiliana na majanga mkuu.sio kila lawama mnambebesha mwanamke khaaaaaaaaaa
 


Kanga ya nini?Mwingine anabeba ili na yeye aonekane mwanamke kwa vile kaaminishwa kubeba kanga ndio kutamfanya aonekane mwanamke na hasa mbele ya wanaume.

Ingekuwa kanga itakuzuia na wezi au matapeli hapa bongo kweli,vinginevyo hata mwanaume anatakiwa ajisitiri.
 
Asante mkuu. kadri mlivyowatendea hao mmenitendea mimi. maneno ya Mungu hayo. wewe utabarikiwa. kanga au mtandio ni wa muhimu wadada.
 
Mkeshaji, kanga/ mitandio tunabeba lkn kwa yaliyomukta huyo dada hata kama angekuwa na kanga angeivaa saa ngapi na tukio limetokea ghafla, ubarikiwe kwa kuokoa maisha ya bidada
 
Mkeshaji,

Napata hisia kama ulimpa huyu dada "Mouth to Mouth" mzee :lol:

Ahahaha!
Kwenye CPR hiyo ni muhimu sana, sema niliweka kanga juu ya mouth kupunguza risk.
Otherwise, ajali kazini mkuu :lol:
 

Pengine wengine wangeelewa zaidi ningeandika hivi:
"Faida za kanga kwa mwanamke ni hizi:
1......
2.....
3.....

Na hasara za kutokuwa na kanga kwa mwanamke ni hizi:
1....
2..... n.k."

Bahati nzuri incidence hii imetokea ndo maana nimeweza/nimekumbuka kuunganisha na matumizi ya kanga kwa mwanamke.
Mwingine angeweza kuelezea maudhui kama haya kwa maneno mengine na kisa kingine penginepo.
 
::: Cardio-Pulmonary U-rescusitation (CPU) :::
kumbe mi ni huduma ya kwanza . . . . :lol:

Mkuu naona umepiga kona halafu kabla haijaguswa na mtu ukawahi kufunga mwenyewe :lol:
 
Reactions: CPU
Wakati mwingine unaweza kudhani watu wanatumia mbinu ya kujifanya wajinga ili kujipatia umaarufu humu, lakini ndo tunawaona wajinga kweli hivyo.

Kwahiyo ameona kutumia busara na hekima hawez kuwa maarufu?
 
Hivi smile kuna mahali mwanamke amebebeshwa lawama hapa? Nijuavyo mimi imeletwa kama ushauri, na ushauri huwa unatolewa bure kuukubali au kuukataa ni haki yako ya msingi....ila pia sio lazima utoe lugha chafu, kama wewe huoni umuhimu wa kubeba kanga au mtandio kwenye handbag yako ni sawa na ungeweza kutufundisha na sie washamba tunaobeba mbadala wake ni nini. Jf ni mahali pa kufundishana na kujifunza hivyo mie binafsi ningefurahi kusikia mwenzetu una mbadala gani..
 



Mko mbali kabisaaaaaaaaaa na maana ya mtoa mada. Yaani mmeelewa kama vile kasema "kutembea na khanga ndio njia pekee ya kujikinga na janga kama hilo". Too low understanding!!

Kaielezea khanga kama mojawapo ya njia ambayo ingesaidia, kati ya njia nyingi ambazo zingeweza kutumika. Ndio maana ktk mkasa huo walimuomba khanga mwanamke mwingine ili kumsitiri mwenzao. So its an advice. You can follow it or not.
Tumshukuru ameokoa maisha ya mwenzetu, hasa mwanamke na pia kasaidia kufanikisha kumsitiri mwili wake.
 

I like and love this comment!
 
hongera sana mkeshaji kwa moyo wako huo wa huruma. Umenikumbusha pale ud udasa kuna mdada alishuka kwenye daladala na kipedo chake cha kaki ,kilikuwa kimelowa damu ya bleed kuanzia hapo mbele hadi nyuma kwenye makalio,yaani full red, ilikuwa ni aibu tupu. Mbaya zaidi hakuwa na kanga wala mtandio, ilibidi akomae hivyo hivyo hadi hall 5.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…