Gwappo Mwakatobe
R I P
- Nov 22, 2019
- 1,796
- 2,345
Awali ya yote niseme kuwa watu kutofautiana mawazo ni jambo zuri na la kawaida sana, ikiwa wataendelea kuheshimiana kwa tofauti zao, yaani kutofautiana pasina kuhitilafiana.
Misimamo ya CHADEMA na G55 ni tofauti ambazo zinazungumzika pasina kuvunjiana heshima na kuhisiana vibaya. Kuitana usaliti, kuhongwa na majina mengine mabaya hadharani, si uungwana kwa taasisi kubwa kama CHADEMA. Hoja zijibiwe kwa hoja ndani ya vikao vya chama na kufikia mwafaka mwema.
Aidha,, tatizo kubwa ni kwamba anachofanya Lissu na kikosi chake ni tofauti na maana sahihi ya kaulimbiu ya "Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi." Yaani "No Reforms, No Election. "Kwanza, uchaguzi haufanywi na matakwa au utashi wa mtu au chama fulani. Upo kwa mujibu wa sheria.
Pili, hakuna mwenye mamlaka yoyote yale ya kuzuia uchaguzi, isipokuwa unaweza kususia (boycott) tu! Hilo naamini Lissu analijua vema. Kwahiyo angesema hivi: "No Reforms, Boycott Election!" Yaani "Bila Mabadiliko, Susia Uchaguzi."
Tatu, Lissu anakosea sana kama anatafsiri kuwa "No Election" humaanisha kuzuia. Maana yake sahihi ni hakuna uchaguzi halali, ni haramu. Hata kama utafanyika utakuwa batili kwa maana ya kuwa ni uchafuzi tu.
Na kama ni kuzuia anakokunadi angesema hivi: "No Reforms, Stop Election!" Japo hakuna mtu au taasisi ya kufanya hivyo kisheria kama nilivyoeleza hapo juu.
Nihitimishe kwa kushauri wanachama na wafuasi wa CHADEMA waseme "No Reforms, Boycott Election." Yaani "Bila Mabadiliko, Susia Uchaguzi." Kuzuia (stop) kutakigharimu chama vibaya na kuwapa sababu ya watesi wao kuwatesa zaidi, tena kisheria!
Mungu atupe hekima na ustaarabu wa kuleta mabadiliko chanya yasiyokuwa na mateso na maumivu. Tayari tumeumia vya kutosha na kuaibika kitaifa na kimataifa.