Ushauri wangu kuhusu maridhiano na kuliponya taifa la Tanzania .

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,530
Reaction score
3,422
Habari wana jf, Huu ndio ushauri wangu kwa Rais Samia , CCM ,Vyama vya Upinzani na watanzania kwa ujumla hususani katika maridhiano na kuliponya taifa kunakozungumzwa .

Kwa katiba tuliyonayo tunategemea sana maamuzi ya Rais aliyepo madarakani na CCM , hata mataifa ya nje hayawezi kutusaidia sana kama baadhi wanavyofikiri .

1.Tuondoe tofauti zetu zote zilizo na wote kuwa Watanzania , awe Kiongozi,MwanaCCM,mpinzani ,mwanausalama, ,mtanganyika,mzanzibar mtumishi wa Serikali au binafsi wote tuwe watanzania.

2.Kesi zote za kisiasa zifutwe na washikiliwa wote wa matukio ya kisiasa na wafungwa wa kisiasa waachiwe huru bila masharti yoyote .
Na wenye uwezo wahusishwe kwenye mchakato wa kupata katiba Mpya .

3.Ufanyike mchakato kabla ya 2029 tuwe tayari tushapata KATIBA MPYA.
Najua hili litakuwa gumu sana kwa CCM, lakini ukweli ni kwa baada ya miaka 100 watanzania wote tuliopo leo hatutokuwepo tuondoe ubinafsi na tufanye kwa vizazi vijavyo .

Kila mtu anatambua CCM hawako tayari kuiachia Nchi na Rais Samia na marais waliopita hawakuwa tayari chama CCM kiwafie mikononi mwao lakini ,lakini sio CCM tu hata CHADEMA tukiingia madarakani itakuwa ngumu kuachia nchi nishauri tu tuweke Utaifa mbele tupate katiba mpya .

Kuna siku niliwahi sema nitawalaumu sana Hayati Mwalimu Nyerere na Hayati Magufuli kwa kutoleta katiba Mpya sababu kwa namna moja au nyingine hawa watu waliona mapungufu, Mwalimu nyerere aliwahikiri kuwepo mapungufu.

Kwa katiba hii mambo mengi tunategemea maamuzi ya watu wachache .
Kwa katiba hii sishauri hata kuandamana tutafute labda njia nyingine, kuna watu watasema ni uoga lakini waliowahi andamana wanaelewa zaidi.

Na huu ndio ushauri wangu , Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.​
 

Attachments

Sawa wakubwa wamesikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…