Ushauri wangu kwa 'Kijana' wa Mzee Kilomoni

ninosi

Senior Member
Joined
Jun 30, 2022
Posts
151
Reaction score
333
Kuna 'Kijana wa Mzee Kilomoni' namuona tangu siku ya jana anajaribu kumtikisa Mnyama. Ndani ya siku 1 kafungua nyuzi zaidi ya 2 akihoji uwekezaji wa Mo katika timu bora kabisa ukanda wa Africa Mashariki na Kati, Simba SC huku akifufua 'nyuzi' za nyuma kwa kupost kuwa amembuka sana 'Mzee wake'.

MASWALI NILIYOJIULIZA:
'Kijana wa Mzee Kilomoni' umejiunga JF tangu 12/10/2017. Tangu kipindi hicho hukuwahi kupost chochote kuhusu mpira wala Simba SC.

1. Tangu jana unahoji kuhusu uwekezaji wa Mo, 'Kijana' hukua na taarifa Mo kakabidhiwa timu tangu 3/12/2017?
2. Kijana kama umemkumbuka 'Mzee wako' si umfuate kwake?

USHAURI WANGU KWAKO:
1. Timing yenu ya kuja kutuvuruga mda huu tukiwa na majambo lukuki ni mbovu mno.
2. Simba SC ya sasa ni IMARA MNO.
 
Hivi inawezekana timu kuvugwa na nyuzi za JF? hivi inawezekanaje hii?
 
Ni wa kupuuzwa hao hawana jipya. Timu inaonakekana uwekezaji wake,wachezaji wake,mambo yanaenda vzr yy anahoji bilioni 20,hivi Mo kashqfanya mangapi Simba mpk sasa au anataka kila kitu anachofanya atangaze. Upuuzi mtupu
 
Hivi inawezekana timu kuvugwa na nyuzi za JF? hivi inawezekanaje hii?

Tetesi za Kocha Nabi kufukuzwa zilianzia wapi? Na baada ya kama masaa kadhaa zilitapakaa kila kona kwa kiwango ambaocha Uto ilibidi waje wakanushe.

Mkuu JF ni dude kubwa sana.
 
Ni wa kupuuzwa hao hawana jipya. Timu inaonakekana uwekezaji wake,wachezaji wake,mambo yanaenda vzr yy anahoji bilioni 20,hivi Mo kashqfanya mangapi Simba mpk sasa au anataka kila kitu anachofanya atangaze. Upuuzi mtupu

Umenena vyema Mkuu.
 
Sikiliza wewe kijana wa Moo! Sisi mashabiki wa simba tunataka mtuambie zile bilioni 20 zimewekwa kwenye akaunti gani ya Klabu! Tumechoshwa na janja janja za mwekezaji!

Na msipotuweka wazi kuhusu hizo hela, tutaandamana mpaka nyumbani kwa Mzee Kilomoni ili kumshinikiza kuchukua timu.
 
Ni wa kupuuzwa hao hawana jipya. Timu inaonakekana uwekezaji wake,wachezaji wake,mambo yanaenda vzr yy anahoji bilioni 20,hivi Mo kashqfanya mangapi Simba mpk sasa au anataka kila kitu anachofanya atangaze. Upuuzi mtupu
Nakuapia mwaka huu hauishi! Mzee Kilomoni lazima airejesha timu mikononi mwetu wanachama na mashabiki! Haiwezekani mwekezaji aendelee kuindesha timu kijanja janja tu.
 
Kumbe mnaitamani sana Simba maana nawaona watopolo wote kila anayepost anajiita mwana Simba. Karibuni Club ya wastaarabu. Huko mlipotea kila siku makasiriko tu mwishowe mtapata maradhi yasiyoambukiza lakini yasiyotibika.
 
Nakuapia mwaka huu hauishi! Mzee Kilomoni lazima airejesha timu mikononi mwetu wanachama na mashabiki! Haiwezekani mwekezaji aendelee kuindesha timu kijanja janja tu.
Nyie watu wabaya sana,mlimchochea Mzee wa watu akalianzisha yalipomkuta yakumkuta mkapiga kimya. Sasa hivi anajiuguza kiharusi chake hataki tena kuwasikia Utopolo.
 
Mo ataondoka, Barbara ataondoka... uhuni kwenye timu hautavumilika, we subiri na kuona.. hakuna maneno mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…