Ushauri wangu kwa Rais Samia kuhusiana na namna ya kumkomboa kijana

Ushauri wangu kwa Rais Samia kuhusiana na namna ya kumkomboa kijana

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,992
Reaction score
5,665
1000003917.jpg

Raisi nianze na kutoa sababu ya umasikini kuendelea kututafuna Watanzania ni kwasababu ya Serikali kusahau kuwainua vijana.

Vijana wa Tanzania hatuhitaji sana kukaa darasani bali tunahitaji mitaji kwasababu tumezaliwa na vipaji. Vijana wengi wa Tanzania tunafanya kazi kwa kutumia vipaji vya kuzaliwa kwasababu ya gharama za mafunzo kuwa ghali sana na sisi wenyewe ni mashahidi kuwa hapa Tanzania tuna matajiri wengi ambao hawajasoma bali wao waliamini zaidi kwenye mtaji

Tunaomba unapotembelea mataifa makubwa tengeneza mfumo wa kijana wa kitanzania kukopesheka kwa urahisi. Sisi ni mashahidi kuwa kuna mkopo wa Halmashauri wa kumwinua kijana lakini ukweli ni kuwa fedha hizo ulizopeleka Halmashauri zimekaliwa na Wazee ambao ni watumishi wa idara hizo za mikopo na vijana wanapojaribu kukopa huwa wananyimwa kwa makusudi ili hao wazee waendelee kuzikalia na kuzitafuna.

Ombi letu kwako Mh raisi, tunaomba tengeneza mfumo wa vijana kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa na Nchi na katika kila ngazi iwe na Mwenyekiti wa vijana na Makamu ambao ni vijana jinsia ya kike na kiume na sio wazee, kwasababu vijana hawapendi kusimamiwa na wazee na wala wazee hawapendi kusimamiwa na vijana, kisha Serikali itoe mkopo ambao utawafikia vijana moja kwa moja pasipo kubabaishwa na Ofisi kama inavyofanyika sasa

Ni vyema kila ngazi kwanzia Kijiji, Kata, Wilaya na Mkoa iwe na account ya bank iliyoundwa na Serikali ambayo itatumika kutoa Mkopo wa Serikali moja kwa moja kwa vijana hao na kupokea Marejesho yao. Ikiwezekana kila kijana akopesheke yeye binafsi kwasababu mkopo wa vikundi huwa haufanikiwi na mwisho wake ni lawama kwa wanavikundi zinazotokana na dhuluma

Account hizo zisimamiwe na Wenyeviti wa vijana, na pale mkopo unapotakiwa kutolewa basi usainiwe na Wenyeviti wao

Katika vijana waunde team ya kutembeleana na kukagua maendeleo ya fedha wanazopewa na wale vijana wanaofanya vizuri waendelee kupandishwa daraja la kukopeshwa ili baadaye wafikie sifa ya kukopesheka bank

Mh raisi endapo ushauri wangu utafanyiwa kazi basi tutegemee kutokomeza umasikini Tanzania ndani ya muda mfupi kwasababu endapo 70% ya vijana wa Tanzania watakuwa na uwezo wa kumiliki 5,000,000 kama mtaji inamaana kwamba tayari Tanzania tutafanikiwa na kuushinda umasikini

Hizi 5,000,000 vijana hawawezi kuzipata kwa mkupuo bila Serikali kutushika mkono kupitia mfumo huu wa mkopo ninaoshauri hapa ambapo wataanza kukuzwa kuanzia chini ili wapande taratibu na kufikia malengo makubwa

70% ya vijana watakapomiliki 5,000,000 watakuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa vijana wenzao na mwisho nchi itafanikiwa haraka

Vijana waliomaliza vyuo na wengine waliokosa mikopo wanazurura mitaani na kupoteza nguvu kazi pamoja na kuchelewesha maendeleo na hii yote ni kwasababu hawana mitaji.

Vijana watakapopata mitaji watazalisha pesa nyingi na nchi itaweza kujiendesha yenyewe na maendeleo yatapatikana kwa haraka.

Ikumbukwe kuwa nchi haiwezi kufanikiwa haraka endapo idadi kubwa ya vijana haizalishi pesa
 
Back
Top Bottom