Ushauri wangu kwa rais wa Yanga Hersi kuelekea mechi ya fainali

Jbst

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2020
Posts
1,971
Reaction score
4,085
Kwanza kabisa piga marufuku wanasiasa na wasaka sifa kuja kambini kwa kisingizio cha kuleta hamasa kwa wachezaji. Kuna watu wanataka kuitumia Yanga kama mtaji wao kisiasa hawa ni wa kuwaeupuka kuelekea mechi hii muhimu.

Sote tumeona kinachotokea mechi za taifa stars wanasiasa wanaitumia team ya taifa mwisho wa siku mambo yanaharibika, tafadhal wanasiasa kaeni mbali na Yanga, hii team haiitaji kuhamasishwa na wana siasa ili ishinde, hata hizo pesa za kila goli ni upuuz tulipaswa kuzipuuza hazina maana yoyote sasa milion 20 wanagawana bei gn wachzaji?

Yanga imetumia gharama kubwa kutengeneza kikosi cha ushindi na benchi la ufundi imara kufikia mafanikio haya kwahyo hatuhitaji hamasa za wanasiasa kushinda mechi. Mpendwa rais wetu usiwaonee haya kuwachana hata huyo FA mchane ni marufuku kwenda kambini au popote kuwakarbia wachezaji kabla ya mechi.

benchi la ufundi waachwe wafanywe kazi yao hao wote wanaojiita wahamasishaji waende uwanjani kushangilia team hii ni hamasa tosha. Na baada ya game ndo wapewe nafasi kuzungumza na wachezaji kama watataka ila sio sasa.

Hata hii tabia ya mgeni rasm ni ya kishamba tunapaswa kuachana nayo mara moja,hata huyo karia apigwe marufuku kutaka kuleta hamasa yoyote kuelekea mechi hii.

Mpira na siasa vitu tofauti kabisa, nashangaa rais unakuwa muoga unawaonea haya badala uwachane!!
 
Ni kweli kabisa baadhi ya Wana siasa wetu siyo wa kuwaamini kabisa. Haswa huyo uliyemtaja ni mnazi wa mkubwa wa upande wa pili anaweza akafanya lolote lile.
 
Tukubaliane tu huo uwezo wa kuwapiga marufuku hao wanasiasa kwenda kambini, hana.

Hivi inawezekana kweli Waziri ametumwa na Rais wa nchi kupeleka salamu za kuitakia ushindi timu! Halafu Injinia Hersi Said kirahisi tu ampige marufuku!! Kweli inawezekana?
 
Wimbo wa jumapili uwe ule ule kivumbi na jashooo . Leo ndo leo leo kivumbi na jashooo
 
Kuna watu hapa hawajui haswa raisi ni mtu gani na ana nguvu gani. Watu hawa hawajawahi kushiriki hata mbio za mwenge wakajionea
 
Kwanza kabisa piga marufuku wanasiasa na wasaka sifa kuja kambini kwa kisingizio cha kuleta hamasa kwa wachezaji. Kuna watu wanataka kuitumia Yanga kama mtaji wao kisiasa hawa ni wa kuwaeupuka kuelekea mechi hii muhimu...
Kabisa Yani wachezaji na benchi la ufundi wawe bize na mechi... Wasirusiwe kukutana na mtu yyt asiyehusika na soka
 
Unachosema kiliwahi kusimuliwa vizuri Sana na Mohamed Mwameja kuhusu Mechi ya fainali Kombe la CAF 1993 dhidi ya Stella Abidjan ya Ivory coast. Mkesha wa Mechi Wachezaji waliamshwa zaidi ya mara 5 kusikiliza hamasa za Viongozi. Mwameja anasema kuna kiongozi alipeleka hamasa ya maneno za 8 usiku. Imagine Mtu umelala, ghafla SAA 8 usiku unaamshwa uambiwe tu umuhimu wa kushinda Mechi utadhani wewe hujui?
Hili si la Injinia Hersi, hili ni la wanasiasa wenyewe. Iacheni timu itulie maana iko vitani, ikishashinda mtaiita kuipongeza Kwa wakati wenu. Salaam zenu za hamasa mnaweza kuwapa viongozi wao au mkaitisha Press mkauambia Umma Kwa niaba yao watafikishiwa. Ninajua wanasiasa mnataka kutumia Kila fursa kujijenga, lakini mara nyingi ujengaji wenu unaishia kubomoa.
 
Yanga timu yetu sisi wanasiasa (CCM) we ni nani mpaka utufungie vioo kwenye timu yetu?? kaanzishe ya kwako ndo uweke hizo sheria zako uchwara..
 
Karai la tff jinga jinga sasa hivi linajifanya linataka kuwa karibu na YANGA...
Watuachie YANGA yetu NABI, Carze na akina Mwamnyeto wanatosha kujipa hamasa wao wenyew...
 
Umeandika point tupu lakini tatizo huwezi kuwazuia wenye timu ndio shida inakuja hapo.

Simba na Yanga ni timu zinazomilikiwa na serikali, sijui tuwaambie Mara ngapi ili muelewe?

Matapeli wote wanaodhurumu na kukwepa kodi ndio serikali huwa inawapa dhamana ya kuzihudumia timu hizi ili waendelee kuwa Salama.

Kuna mshamba kutoka Chato hakuwahi kuijuwa siri hii ndio ukaona anawasumbuwa matapeli waliopewa jukumu na serikali kuzihudumia timu zake.
 
Umeongea ukweli ingawa umewasilisha kiutani utani flani ivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…