Mapambano Yetu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 1,130
- 2,102
Katiba ni mali ya watanzania wote bila kujali dini, kabila, umri, na elimu ya mtu. Hivyo ni vema serikali ikahakikisha maridhiano kabla ya kuirejesha kwa wananchi ili ipigiwe kura. Haitakuwa vyema kura ya maoni iliyohairishwa ikarejeshwa na kupata kura nyingi za "HAPANA". Ili kuepuka hayo, binafsi naishauri serikali kufanya yafuatayo:
1. Makundi yanayopingana yapatanishwe kwanza ili kuweka mambo sawa. Hapa namaanisha serikali ifanye UPATANISHO WA KWELI baina ya waislam na wakristu. Yale aliyokuwa akiyafanya Pinda ni vichekesho vitupu. Huwezi kukutanisha viongozi wa dini ambao unajua dhahiri kuwa ni wafuasi wako kisiasa na ni wanaccm watiifu ukasema kuwa umefanya upatanisho. Inabidi kukutanisha viongozi wa Waislam wenye msimamo mkali, Viongozi kutoka jukwaa la Wakristu na makundi mengine ya dini bila kujali itikadi zao kisiasa ili kufanya upatanisho wa kweli.
2. Serikali ihakikishe imefanya upatanisho wa kisiasa baina ya vyama vyetu. Pale palipo na makosa yarekebishwe kabla ya kurejea kwenye kura ya maoni. Tutafurahi kama serikali, ccm na ukawa watakaa meza moja na kufanya makubaliano yenye tija na mwelekeo wa kitaifa bila kujali itikadi za vyama vyao.
3. Tume ya Uchaguzi iepuke kutumiwa kama mtaji kwa baadhi ya vyama vya siasa (ccm). Kabla ya kutangaza tarehe ya kura maoni tume ijiridhishe kwanza kuwa kila kitu kiko sawa. Mfumo wa kuwafurahisha watawala haufai kwa dunia ya sasa. Zaidi itakuwa ni kujidhalilisha kama ilivyodhalilika this time.

NAWATAKIA UTEKELEZAJI MWEMA
"MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBAR"
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"