Ushauri wangu kwa serikali

Ushauri wangu kwa serikali

Nasri Benson

Member
Joined
Sep 15, 2016
Posts
63
Reaction score
77
Ushauri wangu kwa serikali
1. Wizara ya Nishati, EWURA na TANESCO
.
( A ) Kwa kuwa ripoti zao zinaonyesha umeme uliopo ni mwingi kuliko mahitaji basi ni rai yangu washushe bei ya kuingizia umeme kuwa TZS 27,000/= kwa maeneo yote nchini ili kila mmoja amudu na Faida yake ni kwamba shirika litapata faida kubwa kwa kuwauzia umeme watu wengi kuliko kukomaa na wateja wachache na kuwaacha wengi zaidi walioshindwa kumudu gharama za service line.

( B ) watumie Dam zilizopo kutengeneza mabwawa mengine( waste water) mfano la mwalimu Nyerere wakahifadhi maji kwa kujenga bwawa lingine kama shida ni slop watumie umeme huo huo kufunga pump za kujaza maji ili ikifika kiangazi main dam lilipungua maji basi watumie bwawa la pili kuzalisha umeme faida ni kwamba wataweza kuya control maji ambapo yatapunguza athari kwa jamii mfano yale mafuriko.

( C ) Watengeneze customer portal ili mteja aweze kufuatilia matumizi yake hata akiwa mbali mfano wa bank statement ambapo kwasasa ni mpaka mteja afike ofisi ya tanesco hii itawasaidia hasa wenye viwanda vidogo mfano mtu anamiliki mashine ya nafaka Mwanza lakini anaishi Morogoro inawezekana msimamizi wake ananunua umeme bila taaarifa ikiwepo hii itasaidia, ikiwezekana zaidi waje na mfumo wa smart meter ili mtu aingize umeme popote atakapokuwa mfano ilivyo kwa ving'amuzi.

( D ) Kwasasa kuna mradi wa nguzo za zege ushauri wangu kwa miradi mipya ni bora wakatumia hizo za zege kuliko za miti ambapo baadae watakuja wabadilishe hii itakoa gharama nyingi ikiwemo nguzo zenyewe, kulipa wakandarasi na waya mpya

2. Uchukuzi, Biashara na Viwanda.
Wapunguze ushuru wa kuagiza magari ya miaka ya karibuni mfano 2015- to current na waongeze ushuru kwa 2015 kurudi nyuma ( bei ya gari unaweza kuta 3m lakini kodi ni 10+m unbelievable) lengo ni kupunguza wingi wa magari mabovu nchini ambapo asilimia kubwa ajari nyingi zinachangiwa na ubovu wa magari.

Au wafanye jitihada kampuni za magari ziunganishie hapa hapa nchini mfano walivyofanya truck (hizi za howo) licha ya kupunguza magari mabovu itachangia kukuza mapato kwasababu watapata kodi nyingi hasa kwenye mafuta, kuwa na utitiri mwingi wa kodi ambao unasababisha mfano kuingizwa kwa magari 1000 ndiyo utapata kodo nyingi za bandari na tra lakini ni tofauti yakiingia magari 10000 utatoza import fee ndogo lakini utakusanya pakubwa demand ya fuel, vipuri na spear itaongezeka ko watapatia kodi huku
 
Back
Top Bottom