Ushauri wangu kwa wana ndoa wenzangu

Ushauri wangu kwa wana ndoa wenzangu

IJIGHA NDIO HOME

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2019
Posts
760
Reaction score
823
Kwanza mm sio muumini wa watu kupeana taraka.pili ndoa sio Jambo la kukurupuka tu ndugu zangu.nitaanza kuwapA ushauri wanaume;

*Jamani tupende kupunguza na kudhibiti hasira zetu tambueni pia kua wanawake nao wameumbiwa hasila

Unapochukua maamuzi magumu fikilia mala mbili michepuko sio mchongo,nije kwenu wanawake Tambueni mamlaka ya waume zenu.

Mume ni kiongozi jibizana nae kwa heshima na adabu,hakuna haki sawa kwenye ndoa.kipato isiwe sababu ya kumdhalau mwenzio,michepuko sio mchongo.

Sina mengi natumai wahusika wamenielewa
 
Mpaka kufikia uwamuzi wa talaka Kwa wanandoa ujue si jambo dogo!

Na Mimi huwa na waambia watu facts au scenario huwa hazifanani.

Kwa hiyo hatupaswi kuwa na conclusion ya aina moja!
 
Ni ujinga kung’ang’aniza na kulazimisha wanandoa waendelee kuishi pamoja iwapo mmoja wao hasa alietendwa nafsi yake inakataa kurejea ndoani.

Au wote 2 wako tayari kuachana halafu wapambe wanajifanya kutafuta suluhu!

Kama uelewa ukiimarika kwenye jamii matatizo mengi uataepukika ikiwepo mauaji na ulemavu wa kudumu utokanao na wivu wa mapenzi.

Kuachana kunaepusha madhara mengi sana kwenye mahusiano ya ndoa.

Jamii inahitajika elimu kuhusu hili jambo.
 
Ule upendo wa mwanzo huwa unaenda wapi mpaka watu kuchukiana mpaka hata kuuana ?

Sasa upendo si unatakiwa kuwa wa pande zote 2 au ni upande mmoja tu ndio upende na mwingine uwe unaumiza mwenzie ?

Ni kweli Imeandikwa upendo huvumilia lakini unavumilia Mwaka wa 1, 2 mpaka 10 Yani maisha yote mwanandoa mmoja awe anavumilia tu na mwingine kazi yake kufanya uasi akijua for granted atavumiliwa na kusamehewa?
 
Mpaka mmefikia maamuzi ya kukaa pamoja ina maana Kila mmoja alikubali kuyabeba mapungufu ya mwenzake (kumfichia madhaifu), ila kuja kutengana maana yake ni nini Sasa ?
 
Mpaka mmefikia maamuzi ya kukaa pamoja ina maana Kila mmoja alikubali kuyabeba mapungufu ya mwenzake (kumfichia madhaifu), ila kuja kutengana maana yake ni nini Sasa ?

Mapungufu yakunebana Ni yale ambayo hayatokani na makusudi.
 
Mpaka kufikia kujirudiarudia lazima kuna sababu na huenda 'mwandani' wake akawa sehemu ya sababu au hata sababu yenyewe kwa kujua au kutokujua.

Huenda lakini sio lazima iwe hivyo wakati wote.

Ikifika hapo sasa ndio hutegemea scenario na scenario!

Huwa hazifanani na sensitivity zake!

Huwa sio rahisi kama hesabu za 1 + 1 = 2.

Halafu watu wanakosea kuforse suluhu wakati moyo wa aloumizwa ukiwa bado na majeraha!

Jamii inahitajika elimu ya mambo ya mahusiano na psychology.
 
Watu kulazimisha suluhu sidhani kama inaweza kuwa tatizo, japo ndoa ni ya wawili ila kuna ambao wana maslahi ya moja kwa moja na hiyo ndoa, mnapoivunja na wao mnawaweka pagumu mfano watoto au hata familia zenu mbili.

Kuivunja bila kuangalia au kupima hiyo athari kwa hayo makundi mengine huenda ikawa ubinafsi.
 
Back
Top Bottom