Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,466
Mkandara,
Sioni ubishani tulikuwa tunaelimishana na kufafanualiana habari na ushauri wako kwa kijana wetu ZZK. Ni wazi kila mtu anajinsi ya ufahamu na chanzo cha habari ikumbukwe tu ZZK ni mwanasiasa wa chama maarufu. Sioni kama watu wanachuki naye bali wengi wanampenda sana na wanamategemeo naye makubwa ndio maana wana hoji na kuhoji na kuhoji.
Naona kuna wenye nia mbaya sana na CDM kwani wanapenyeza hata ambayo hayahusiki, Kama nia ni kumshauri usikatae na mawazo ya wengine, ZZK anafahamiana na wengi na kafanya kazi na wengi kwenye hii siasa yetu.
Ushauri wako kwa upande ni mzuri na sehemu nyingine itabidi ZZK aamue mwenyewe.
Mkubwa Mkandara lazima wote tukubali kuwa hakuna mtu alizaliwa anapenda fedha ila maisha na mahitaji ndio yanasukuma uhitaji wa fedha , sidhani kama kuna mtu anayependa kuwa masikini na sitaki kumwona mtu wa hivyo. Huwezi kuwa na uhakika na rushwa na kupenda fedha kwa mtu ila mtu mwenyewe.
Wote tunaamini (imani) kwamba kijana ni safi ila sidhani kama ni sahihi kuchukua nafasi yake kumtetea mimi nikiwa kama mwana CDM na rafiki wa ZZK ningependa yeye mwenyewe ajitete kuliko kuwa kama CCM ambao huwa wanateteana hata kwenye ukweli. Kama ZZK ni msafi hakuna la kuogopa wala hakuna sababu ya kuogopa wanaojadili.
CDM lazima ijengwe kwenye misingi ya uwazi na ukweli na ninamsifia ZZK kuweka wazi kwamba yeye yuko tayari kuchunguzwa na yeyote.
Swala la makundi ndani ya CDM nafikiri ni fikra na baadhi ya watu kutaka kuwavuruga na kutengeneza makundi kwa hisia , ni kweli kuna wenye misimamo tofauti lakini sitegemei CDM viongozi wafikiri sawa hakuna zidumu fikra huku, kuna uwanja huru wa maoni na fikra.
Misuguano hakuna mahala ambapo haipo ila bado haijawa tatizo ndani ya chama.