Ushauri wangu kwa Zuberi Zitto Kabwe

Ushauri wangu kwa Zuberi Zitto Kabwe

Mkandara,
Sioni ubishani tulikuwa tunaelimishana na kufafanualiana habari na ushauri wako kwa kijana wetu ZZK. Ni wazi kila mtu anajinsi ya ufahamu na chanzo cha habari ikumbukwe tu ZZK ni mwanasiasa wa chama maarufu. Sioni kama watu wanachuki naye bali wengi wanampenda sana na wanamategemeo naye makubwa ndio maana wana hoji na kuhoji na kuhoji.

Naona kuna wenye nia mbaya sana na CDM kwani wanapenyeza hata ambayo hayahusiki, Kama nia ni kumshauri usikatae na mawazo ya wengine, ZZK anafahamiana na wengi na kafanya kazi na wengi kwenye hii siasa yetu.

Ushauri wako kwa upande ni mzuri na sehemu nyingine itabidi ZZK aamue mwenyewe.

Mkubwa Mkandara lazima wote tukubali kuwa hakuna mtu alizaliwa anapenda fedha ila maisha na mahitaji ndio yanasukuma uhitaji wa fedha , sidhani kama kuna mtu anayependa kuwa masikini na sitaki kumwona mtu wa hivyo. Huwezi kuwa na uhakika na rushwa na kupenda fedha kwa mtu ila mtu mwenyewe.

Wote tunaamini (imani) kwamba kijana ni safi ila sidhani kama ni sahihi kuchukua nafasi yake kumtetea mimi nikiwa kama mwana CDM na rafiki wa ZZK ningependa yeye mwenyewe ajitete kuliko kuwa kama CCM ambao huwa wanateteana hata kwenye ukweli. Kama ZZK ni msafi hakuna la kuogopa wala hakuna sababu ya kuogopa wanaojadili.

CDM lazima ijengwe kwenye misingi ya uwazi na ukweli na ninamsifia ZZK kuweka wazi kwamba yeye yuko tayari kuchunguzwa na yeyote.

Swala la makundi ndani ya CDM nafikiri ni fikra na baadhi ya watu kutaka kuwavuruga na kutengeneza makundi kwa hisia , ni kweli kuna wenye misimamo tofauti lakini sitegemei CDM viongozi wafikiri sawa hakuna zidumu fikra huku, kuna uwanja huru wa maoni na fikra.

Misuguano hakuna mahala ambapo haipo ila bado haijawa tatizo ndani ya chama.
 
Nicholas, For the last time nakwambia hivi soma tena mada yangu hakuna mahala nimezungumzia TUHUMA isipokuwa hali halisi ambayo Zitto anaifanya kusimamia sera za CCM pale anapoona anaweza kuleta mabadiliko through sera mbovu. Na nimeshauri ajipange na team yake kupinga sera mbovu za CCM badala ya kufikiria he can make them change what they stand for!..

Maelezo hayo juu hayana kabisa TUHUMA za watu ama magazeti kwa sababu vitu vyote unavyomlaumu wewe ni tuhuma zinazo endeshwa na watu wasiompenda na wewe mmoja wapo maana huna facts. Nimekuuliza vizuri tu toka lini mtu anayetuhumiwa ndiye anatakiwa kujieleza ili kufuta tuhuma hizo wakati kisha sema sihusiki ktk vyombo vya habari. Mnasema anapenda rushwa nimesema sio kweli, naye kajibu hivyo hivyo lakini bado hamtaki kuamini..Well kama huna mafaili yake unakataa kitu gani sasa? It's my guess u have facts kuhusu Zitto na rushwa na tamaa mnayozungumzia!.

Now, to declare ana nia ya kugombea Urais, sio kosa na nimekuuliza kosa gani?..hukujibu isipokuwa unarukia yale uyatakayo..japokuwa nina hakika akisema Dr.Slaa wakati wowote ule utamuunga mkono na wengine wote wanaomchambua Zitto kwa kauli ile kwa sababu mmezoea Usiri wa CCM kupitia CC na mafia yake. Labda niseme pia kutotangaza nia yake ya kugombea tena Urais inaweza kuwa ni makosa vile vile maana kuweka nia inawajenga wanachama nyuma yake badala ya hizi kelele mnazopiga humu. WE need a leader ktk harakati zozote zile, na ifahamike wazi nani anatuongoza ktk mapambano haya ili awe kioo chetu.. Kukosekana kwa kiongozi ndio maana kila mtu analoloma anavyotaka..

Again unataka kuzungumzia scandals za Zitto anzisha mada yako nitakuja huko lakini hii inahusu mchango wake kwa chama katika kuzitangaza, kuzitetea na kuzinadi SERA za Chadema, na atashirikiana na CCM tu pale CCM na CDM wamekubaliana ushirika kwa muafaka wa kisera ktk utekelezaji wa mikakati ya maendeleo. Haya yote ni katika Ujenzi wa taifa kwa kutumia sera za chama chake kukosoa mabaya ya CCM badala ya kujitenga kutafuta Umaarufu.

Kwa nini nimezungumzia KUTENGANA, ni kwa sababu kutengana kuna jumuisha pande mbili sisizo kubaliana. IT TAKES TWO TO TANGO, laa sivyo ingekuwa upande mmoja unanyenyekea. Na ukinisoma vizuri pale nilipoweka mafaili nimesema wazi kwamba jaribio lile lilishindikana kukisambaratisha chama isipokuwa kuharibu mahusiano kati ya Zitto na Mbowe. Nasema haya kwa sababu najua kilichofanyika na najua kwa kirefu Zitto ana habari zipi na Mbowe ana habari zipi na nimesema hizi zote zilipikwa kuhakikisha wana kigawanisha chama. They never showed up to deny this fact. WEWE pamoja na kuwepo CDM - HUJUI kitu na hujui minuso ndio maana unashindwa kuelewa mambo yanayokwenda chini ya ardhi.

- Nimemaliza - HUTAKI UNAACHA!
 
Mengi yamesemwa hapa,natumaini imekua shule tosha kwa Zitto,wanasiasa vijana na kwa uongozi wa CDM. Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu.
 
Basi wewe chukua hiii

http://www.youtube.com/watch?v=pI_3Sw5T80Y&feature=youtube_gdata_player
 
Katika wabunge vijana niliokuwa nawavulia kofia ni pamoja na Mheshimiwa Zitto Kabwe, tunakumbuka jinsi awamu yake ya kwanza ya ubunge alivyokuwa akijenga hoja vizuri na hadi kuna wakati alifikia kusimamishwa ubunge kwa ajili ya ujasiri wa kusimamia msimamo wake. Lakini kwa sasa tumeona wabunge vijana wengi, wamekuja juu na tayari wanamfunika Zitto Kabwe. Najua Zitto Kabwe ameweza kufanya mambo mazuri na kuonesha mfano kuwa vijana wanaweza katika kuongozo lakini nakiri na ningependa sio Zitto tu, na wapenzi wake wengine wakiri kuwa Zitto kiasi amepwaya katika siasa mwaka huu. Mwaka huu nimeshuhudia Zitto akipotoka kwa baadhi ya mambo mfano:

1. Wakati akisoma maoni ya upinzani kuhusu bajeti ya Serikali aliharibu na ndiyo maana alitoa nafasi kwa Gamba Mwigulu kuichana chana bajeti mbadala ya upinzani. Hapa hata yeye alikiri kufanya makosa.
2. Alikurupuka kutaka kuingilia sakata la TANESCO ambalo tayari lilishaanza kufanyiwa kazi na mamlaka ingine, hii pia alijitetea sana na kuonekana kubadilika msimamo na hadi kutishia kwamba yeye yupo tayari kuachia ngazi ili ainusuru Kamati yake. Ikumbukwe kuwa wakati akisema watafanya uchunguzi alikuwa kama anaona TANESCO wanaonewa, baadaye akageuka eti hakuwa na maana hiyo.
3. Amekuwa akituhumu kuna watu wanataka nafasi zake, ya Uenyekiti wa Kamati, Usaidizi Kuongoza Kambi ya Upinzania bungeni, na kuzengea ugombeaji wa Uraisi mwaka 2015.
4. Amekuwa anatishia na kutaka kuogopwa, kumbuka hapa pia anatuhumiwa kumwandikia ujumbe wa simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kwamba yeye "hana bei".
5. Ameshindwa kueleweka katika maelezo yake ya hivi karibuni alipojaribu kuelezea sakata la yeye kutajwa kufagiliwa njia ya uraisi 2015 pale ilipoandikwaa magazetini, n.k, kutokana na tamasha la wasanii lililofanyika Kigoma.
6. N.K.

And the list goes on and on....

My advice: Zitto ajiangalie upya kwani inawezekana ndiyo anasererekea bondeni.
 
zito nakushauri urudi ccm na ukagombee ubunge kwa kupitia huko au vyama nipya vilivyoanzishwa na ccm kwa ajili ya kuikabili chadema ambavyo ni chauma ,adc na vingine wanavyovijua wao. nasema hayo sababu nyingi lakini nitasema chache.

1.wakati viongozi wa juu wote wa chadema wanapambana kwa kutumia m4c zito haujaonekana hata kwenye mkutano mmoja ikiwa kama ni kutotaka kutamka maneno ya kuwaudhi waliokutuma kuichafua chadema.

2.zito unapopeleka hoja yoyote bungeni inakuwa ya kujijenga binafsi na si kwa maslahi ya wanyonge wengi na wabunge wa upinzani hususani chama chako na hii ni pamoja na kutokutoka nje ya ukumbi wa bunge pale chadema wanapofanya hivyo kwa maslahi ya chama chao.

3.umejisifu sana kuwa wewe ni muadilifu na unao uwezo wa kuwa rais wa nchi 2015 kwa hili umekosea maana njia uliyoitumia ni mbovu sana maana kuna vikao vya chama ambavyo ungevitumia kueleza hoja yako lakini kwa kutumia waandishi wa habari na bunge na vijana wako wa kigoma halitakusaidia kufika huko maana nyuma yake inaoonekana kuna baraka za bwana mkubwa ili muivuruge chadema.

4.taarifa zisizo rasmi zinaonyesha urafiki wako wa karibu na jakaya na ridhiwani ni mashaka makubwa sana maana hakuna sehemu yoyote ambayo umemlaumu rais wa nchi kwa udhaifu wake bali amekutumia kumdhalilisha waziri mkuu kwa maslahi ya ikulu na si kwa upinzani unaposema serikali haiko makini bado unaficha kumtaja jakaya moja kwa moja sababu ya agenda zenu za siri ambazo wana ccm na wanachadema wengi wameliona.

Umeingizwa kwenye orodha ya wala rushwa wabunge kwa makusudi tu kuichafua chadema na si vinginevyo na hili unalijua vizuri.sidhani kama kupitia chadema utafanikiwa ndoto zako maana chadema wako makini ndio maana hakuna kiongozi wa juu wa chama aliyejibu hoja zako za kuutaka uraisi kiurahisi ushauri wangu kwako utangaze adharani kujiunga kwako na kundi la shibuda nakutakia safari njema.m4c daima.

amuulize waridi kabouru ccm ilimtumia lakini sasa imemtupa kigamboni asijidanganye hata siku moja nguvu aliyopata ni kutokana na ubora wa chadema ila akitaka kuondoka atuchie chadema yetu halafu aende ccm au cuf safari njema zito
 
Vijana acheni kutumika kwa hela ya mboga,mnakaa tumwa humu JF kila kukicha kumpaka matope zitto. Huu mzimu wa urais utawamaliza CDM.
 
mbona ccm mnamuogoga lowasa na huo ni mzimu wa urais au ufisadi nieleze vizuri
 
Arudi kwani kashawahi kuwa CCM?
Watu wa CDM naona kama mnaanza kutengeneza chama ndani ya chama...
 
Sitaki kuamini kama zzk unapakwa matope na wana cdm. hawa ni wafuasi wa nape kaka cdm bado tunakupenda na kila mwanachama wa cdm ana haki ya kuwa mwakilishi wa chama mahala popote pale bila ya kuingiliwa ilimradi asiende kinyume na katiba za chama
 
zito ana kiburi kwa kufikiri wale bongoflavour wake watampeleka ikulu unahitaji baraka za chama sio za kikwete
 
Zito hakuwahi kuwa mwanachama wa ccm, hivyo kusema arudi ccm si sahihi ni bora ungesema ahamie ccm,
Sisi sote ni watanzania hivyo kutofautiana ki-itikadi hakutenganishi utanzania wetu, si dhambi kuwa na urafiki na mtu eti kisa hamko chama kimoja.
Zito bado ni Mwanasiasa safi na makini pale Chadema.
 
Hata sie CCM wazalendo hatumtaki akihamia CCM sie tunaendaaa CDM....kijana kama huyu ndio anawakilisha vijana wa kisanii kwenye siasa za sasa kupitia mingongo ya vijana, uzalendo, na wandishi vijana wa mjini mjiniii.
 
Back
Top Bottom