- Thread starter
-
- #161
Mkuu wangu unachoshindwa kuelewa ni kwamba Ushauri siku zote hutolewa kwa mapenziMwanzoni nilidhani una nia kweli ya kumshauri zito ila baada ya post hii naanza kutilia shaka kama nia yako ilikuwa ni kumshauri zito au ulitaka kupima upepo kama imani ya watu imepotea kwa zito.
Nakushangaa kwamba bado unamtetea zito kuwa anapakwa matope wakati vituko vya zito vinaoneka wazi katika matamko yake. Hata mbumbumbu hapati shida kuelewa anachokifanya zito ktk matamko yake. Kama una nia njema na zito ungana na sie tunaosema wazi kwamba zito anatumiwa na ccm. CCM wanajua kuwa hawana njia nyingine ya kuiyumbisha chadema zaidi ya kumtumia Zito, wanajua kuwa chadema wakimchukulia hatua zito basi ile zana ya ukabila na udini wanayojaribu kuipandikiza itapata nguvu. Bahati nzuri viongozi wa chadema wanalijua hilo na wako makini, wamemwacha zito aendelee kuropoka wakijua wakati utafika ambapo zito atajiangusha mwenyewe na hapo ndio atagundua CCM ni nani.
na sio chuki. Na pengine nikushangae wewe unayetaka nimpe ushauri Zitto kwa hasira na kumsemea hovyo, sijui kama mtu hyo atachukua ushauri wangu..
Zitto ni mwana Chadema, tupo ktk mashua moja na hivyo siwezi kutoa matusi kama nayoyasoma humu isipokuwa kumwelekeza pale napomwona ana mapungufu ama anapotoka kwa moyo mkunjufu kabisa. Na sijui kama umewahi kunisoma ktk mada nyingine niliandika wazi kabisa kwamba CCM wana mtumia Zitto kama weakest link kisiasa kwa sababu Zitto sii mwanasiasa japokuwa anafikiri kisha komaa kisiasa.