Ushauri wangu kwa Zuberi Zitto Kabwe

Ushauri wangu kwa Zuberi Zitto Kabwe

Mwanzoni nilidhani una nia kweli ya kumshauri zito ila baada ya post hii naanza kutilia shaka kama nia yako ilikuwa ni kumshauri zito au ulitaka kupima upepo kama imani ya watu imepotea kwa zito.
Nakushangaa kwamba bado unamtetea zito kuwa anapakwa matope wakati vituko vya zito vinaoneka wazi katika matamko yake. Hata mbumbumbu hapati shida kuelewa anachokifanya zito ktk matamko yake. Kama una nia njema na zito ungana na sie tunaosema wazi kwamba zito anatumiwa na ccm. CCM wanajua kuwa hawana njia nyingine ya kuiyumbisha chadema zaidi ya kumtumia Zito, wanajua kuwa chadema wakimchukulia hatua zito basi ile zana ya ukabila na udini wanayojaribu kuipandikiza itapata nguvu. Bahati nzuri viongozi wa chadema wanalijua hilo na wako makini, wamemwacha zito aendelee kuropoka wakijua wakati utafika ambapo zito atajiangusha mwenyewe na hapo ndio atagundua CCM ni nani.
Mkuu wangu unachoshindwa kuelewa ni kwamba Ushauri siku zote hutolewa kwa mapenzi
na sio chuki. Na pengine nikushangae wewe unayetaka nimpe ushauri Zitto kwa hasira na kumsemea hovyo, sijui kama mtu hyo atachukua ushauri wangu..

Zitto ni mwana Chadema, tupo ktk mashua moja na hivyo siwezi kutoa matusi kama nayoyasoma humu isipokuwa kumwelekeza pale napomwona ana mapungufu ama anapotoka kwa moyo mkunjufu kabisa. Na sijui kama umewahi kunisoma ktk mada nyingine niliandika wazi kabisa kwamba CCM wana mtumia Zitto kama weakest link kisiasa kwa sababu Zitto sii mwanasiasa japokuwa anafikiri kisha komaa kisiasa.
 
Mkandara,

Chama kisiendeshe kwa emotions. Kiendeshwe kwa kutumia katiba ya chama bila kumnyima mtu uhuru wake wa katiba ya nchi au uhuru wa kisheria.

Anayozungumza Zitto hayavunji katiba ya CDM, ya nchi, au sheria. Sasa ni demokrasia gani mnayotaka ya kuendesha nchi wakati ndani ya chama hakuna ushindani?
 
Hukuanza leo wala jana harakati zako kisiasa,najua na wananchi wanajua umefanya mengi ktk siasa za nchi yetu na ni mazuri tu. Mwanaharakati kama wewe si ajabu wala kashangaza unapokuwa na hamu ya kuwa Raisi mwisho wa siku.Na ninawasihi wanaCDM na wananchi kwa ujumla tusimnyooshee kidole kibaya Zitto coz ni hali ya kawaida kabisa na ni haki yake ya msingi kuwa na ambitions za uraisi na mwanasiasa yeyote aliyefikia mafanikio ya juu japo kidogo,hupenda kwenda zaidi ya alipo

Zitto tumekusikia, tumekuelewa na hatukukatazi, lakini naomba uchukue ushauri wangu brother.CHADEMA kiko safarini hivi sasa kuelekea kule vijijini na miji tata kujiimarisha,kinatizamwa kama Chama mbadala kwa sasa na wananchi waliowengi hata baadhi ya wanaCCM.
Unaifahamu mikakati ya Chama ni kwenda kwa kila raia na kueleza dhamira ya chama,kwanini usijikite,ukaungana na wazalendo wenzako ktk chama kupigana na adui kwanza, mkamtoa nyoka ndani ya nyumba,ndipo mkae kitako nani awe mkuu wa nyumba.

Kwa nini usijiunge katika ktk common goal hii! Si muda muafaka kuanza kugawana mali za baba wakati baba ni mgonjwa,yafaa tushukulikie uhai wake kwanza.Au unasahau tunajenga nyumba moja,na fito yako,ya Mbowe,ya Dr Slaa,ya Heche, ya Malya,ya kasulumbai,Msigwa na Sugu,ya Lisu Dr safari,Baregu,ama ya Halima,Wenje na hata Marehem Regia,zote zinahitajika kukamilisha ujenzi.
Tunahitaji fito sasa kwa sasa,sote tulete fito,ukileta rangi saa hizi haitafaa sana japo tutaihitaji baadae ila nahofia ita-expire kabla hatujafikia hatua hiyo.

Mbona muda wa kuzungumzia habari za Uraisi badoooo! Tutumie miaka hii kabla ya 2015 kukipatia ushindi chama mbele ya umma wa watz halafu utatumia nguvu ndogo sana kwenye hiyo dhamira yako ifikapo 2015.
By the way,unafahamu kabisa katiba ya sasa haikuruhusu kugombea,hilo pekee linatosha kukufanya uwe na kiasi na subira pia,lakini si neno.

Kuna Mchakato unaoendelea kuelekea Katiba mpya, mchakato ambao kwa hakika umefanikishwa kwa kiasi kikubwa na Chama chako, suala la umri ktk kuwania uraisi likiwa kipaumbele kwa CDM, hii ni kwa sababu ya imani ya chama kwa vijana wewe ukiwemo. Kwanini usikiweke chama mbele ili kipiganie mazingira ya kisiasa ambayo mwisho wa siku yatakua favor kwako?
Huoni kama unadhoofisha nguvu ya chama kwa kiasi kikubwa?
Usifanye hivyo brother usijeingia ktk historia mbaya kuzuia mabadiliko
Mkuu ushauri mzuri sana huu.

Hapo kwenye bold:ndiyo msimamo wa wengi wetu humu JF.Hata wale wanaopingana na kauli zake za kutaka urais,haina maana kwamba hawajui kuwa ana haki hiyo.Uliyoyazungumza hapo juu ndiyo haswa wamekuwa wakiyasema wengi wetu humu.Sema ni lugha na namna ya kuexplain,lakini kila anayepinga,nyuma yake ukiwauliza sababu wanakupa hizo hizo ambazo umezitoa hapo juu.

Wengi humu hawasemi kuwa "Zitto hafai kuwa rais",bali wanasema "Zitto anafaa kuwa rais,but...",Yani ni yes,but...
Mkandara,nasikitika kusema kwamba ushauri wako haujazingatiwa."A one man army"
399583_477385642282138_137963710_n.jpg
 
Last edited by a moderator:

Muda wa zzk kutangaza urais bado ,ila muda wa heche,deo mushi na kilewo kutangaza kugombea majimbo tayari.
Mnachekesha kweli nyie chadema!
Huu ni mwendelezo ataendelea kutangaza mpaka siku anaenda kuchukua form!
Chuma kimeshika moto sasa!
Atakaejiona anaweza basi akishike aone!
 
Katika wabunge vijana niliokuwa nawavulia kofia ni pamoja na Mheshimiwa Zitto Kabwe, tunakumbuka jinsi awamu yake ya kwanza ya ubunge alivyokuwa akijenga hoja vizuri na hadi kuna wakati alifikia kusimamishwa ubunge kwa ajili ya ujasiri wa kusimamia msimamo wake. Lakini kwa sasa tumeona wabunge vijana wengi, wamekuja juu na tayari wanamfunika Zitto Kabwe. Najua Zitto Kabwe ameweza kufanya mambo mazuri na kuonesha mfano kuwa vijana wanaweza katika kuongozo lakini nakiri na ningependa sio Zitto tu, na wapenzi wake wengine wakiri kuwa Zitto kiasi amepwaya katika siasa mwaka huu. Mwaka huu nimeshuhudia Zitto akipotoka kwa baadhi ya mambo mfano:

1. Wakati akisoma maoni ya upinzani kuhusu bajeti ya Serikali aliharibu na ndiyo maana alitoa nafasi kwa Gamba Mwigulu kuichana chana bajeti mbadala ya upinzani. Hapa hata yeye alikiri kufanya makosa.
2. Alikurupuka kutaka kuingilia sakata la TANESCO ambalo tayari lilishaanza kufanyiwa kazi na mamlaka ingine, hii pia alijitetea sana na kuonekana kubadilika msimamo na hadi kutishia kwamba yeye yupo tayari kuachia ngazi ili ainusuru Kamati yake. Ikumbukwe kuwa wakati akisema watafanya uchunguzi alikuwa kama anaona TANESCO wanaonewa, baadaye akageuka eti hakuwa na maana hiyo.
3. Amekuwa akituhumu kuna watu wanataka nafasi zake, ya Uenyekiti wa Kamati, Usaidizi Kuongoza Kambi ya Upinzania bungeni, na kuzengea ugombeaji wa Uraisi mwaka 2015.
4. Amekuwa anatishia na kutaka kuogopwa, kumbuka hapa pia anatuhumiwa kumwandikia ujumbe wa simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kwamba yeye "hana bei".
5. Ameshindwa kueleweka katika maelezo yake ya hivi karibuni alipojaribu kuelezea sakata la yeye kutajwa kufagiliwa njia ya uraisi 2015 pale ilipoandikwaa magazetini, n.k, kutokana na tamasha la wasanii lililofanyika Kigoma.
6. N.K.

And the list goes on and on....

My advice: Zitto ajiangalie upya kwani inawezekana ndiyo anasererekea bondeni.

hoja zako zimepimwa kwenye mizani zimeonekana
hazina ujazo na ubora unaotakiwa(quality and quantity)
Kajianze upya!
 
zito nakushauri urudi ccm na ukagombee ubunge kwa kupitia huko au vyama nipya vilivyoanzishwa na ccm kwa ajili ya kuikabili chadema ambavyo ni chauma ,adc na vingine wanavyovijua wao. nasema hayo sababu nyingi lakini nitasema chache.

1.wakati viongozi wa juu wote wa chadema wanapambana kwa kutumia m4c zito haujaonekana hata kwenye mkutano mmoja ikiwa kama ni kutotaka kutamka maneno ya kuwaudhi waliokutuma kuichafua chadema.

2.zito unapopeleka hoja yoyote bungeni inakuwa ya kujijenga binafsi na si kwa maslahi ya wanyonge wengi na wabunge wa upinzani hususani chama chako na hii ni pamoja na kutokutoka nje ya ukumbi wa bunge pale chadema wanapofanya hivyo kwa maslahi ya chama chao.

3.umejisifu sana kuwa wewe ni muadilifu na unao uwezo wa kuwa rais wa nchi 2015 kwa hili umekosea maana njia uliyoitumia ni mbovu sana maana kuna vikao vya chama ambavyo ungevitumia kueleza hoja yako lakini kwa kutumia waandishi wa habari na bunge na vijana wako wa kigoma halitakusaidia kufika huko maana nyuma yake inaoonekana kuna baraka za bwana mkubwa ili muivuruge chadema.

4.taarifa zisizo rasmi zinaonyesha urafiki wako wa karibu na jakaya na ridhiwani ni mashaka makubwa sana maana hakuna sehemu yoyote ambayo umemlaumu rais wa nchi kwa udhaifu wake bali amekutumia kumdhalilisha waziri mkuu kwa maslahi ya ikulu na si kwa upinzani unaposema serikali haiko makini bado unaficha kumtaja jakaya moja kwa moja sababu ya agenda zenu za siri ambazo wana ccm na wanachadema wengi wameliona.

Umeingizwa kwenye orodha ya wala rushwa wabunge kwa makusudi tu kuichafua chadema na si vinginevyo na hili unalijua vizuri.sidhani kama kupitia chadema utafanikiwa ndoto zako maana chadema wako makini ndio maana hakuna kiongozi wa juu wa chama aliyejibu hoja zako za kuutaka uraisi kiurahisi ushauri wangu kwako utangaze adharani kujiunga kwako na kundi la shibuda nakutakia safari njema.m4c daima.

pumba ulizojitahidi kuzileta hapa zimethibitisha yafuatayo.
1:hujui ulichokiandika mfano hoja namba nne umeandika nanukuu:inasemekana una urafiki wakaribu na jk na ridhwani.
No research no right to speak hapa sio mahali pakuleta hoja za ufitini na majungu.labda mpelekee slaa atazifanyia kazi maana yeye ni mpenda majungu mzuri.
2:hoja yako ya pili inainyesha umekurupuka na hata katiba ya chadema hujawahi iona hata ina rangi gani acha kuisoma.
Ni wapi katiba ya cdm imeonyesha mahali sahihi pakutolea matamko au kutangaza nia?
au ni tarime maana naona heche alitangazia tarime wala sikukuona kumuandikia utumbo ka huu ulioandika hapa.
Unless ukubaliane na mimi kwamba chadema mna double standard!
3:hoja yako ya tatu umeonyesha uchanga wako wakisiasa(immaturity)mbunge yeyote anapoleta hoja binafsi bungeni kabla hajaiwasilisha inakuwa imeshajadiliwa katika party coccus ya chama husika na kupewa baraka zote na chama.
Endapo ikafanikiwa chama kinapata credit kubwa japo huwezi epuka mbunge husika pia kupata credit zake.
Na ndio maana zitto alipopeleka hoja yakutokuwa na imani na waziri mkuu na baadhi ya mawaziri wabunge wa chadema walikuwa wa kwanza kusaini kabla ya vyama vingine.
Umechemka mbaya!
4:kati ya m4c na zitto nani kamkuta mwenzake kwenye harakati?
Unazungumzia m4c iliyoletwa juzi na wakaskazini kama mbinu yao yakujipatia pesa kiulaini!acha maneno yako wewe!
Zitto kaanza harakati cdm tangu ana miaka 16 we umejiunga chadema kwa njia ya maandamano basi unajiona una uwezo wakumsema zitto!
Mnadhani kusema peoples power ndo kuwa mwanasiasa?
Poor you,with your foolish analysis.
 
Zito ni mzuri sana ktk utendaji hilo halifichiki, analysis zake za kiuchumi zipo deep na critical. He is a creative thinker.

Nadhani anachokosa ni ushauri hasa wanini kisemwe au kifanyike bila kuadhiri sisa za upinzani wala sera za chama ambacho watanzania wote kwaujumla tunakichukilia kama ndo muhimili wa upinzani nchini na ndo chenye mawazo mbadala.

Ushauri wangu..............katika kumuunga mkono Zito ktk mambo mengi anayoyafanya kwania njema namshauri
kwanza katika kutenda kwake na kunena pia ahakikishe yupo ndani ya siasa za upinzani na ndani ya sera za chama.

Pili kama anaona ndani ya chama falsafa yake njema ya kuwawezesha watanzania wote kuwanafursa ya kuzitumia resourses zilizopo haipati suport ya kutosha nivyema akajiunga na chama kingine kuliko kusimama mwenyewe ndani ya chama chenye mamilioni ya watanzania.
Hii itamjengea heshima kubwa kama wanamapinduzi mwnye nia ya kuinua nchi kuichumi.

Tatu kama anabaki ndani ya chama, asimame na wenzake wote, asijitenge na kazi za chama ambazo kwasasa ndizo zinazomuimarisha zaidi kisiasa.

Kila la heri Zito, naamini unapata ushauri mwngi sana ila ktk yote epuka mambo yanayoelekea kukutenga na chama hasa ktk maneno na matendo yako.
 
Mkandara,

Chama kisiendeshe kwa emotions. Kiendeshwe kwa kutumia katiba ya chama bila kumnyima mtu uhuru wake wa katiba ya nchi au uhuru wa kisheria.

Anayozungumza Zitto hayavunji katiba ya CDM, ya nchi, au sheria. Sasa ni demokrasia gani mnayotaka ya kuendesha nchi wakati ndani ya chama hakuna ushindani?
Sizungumziii katiba ya chama, nchi wala sheria bali fursa na nafasi ya Upinzani ktk uwakilishi wake. Nafasi anayoitumia Zitto mara nyngi huonekana kama mgombea binafsi au kuhoji kwa marekebisho ya njia za utekelezaji wa sera wakati anajua fika ni sera mbovu za CCM ndizo zimetufikisha hapa tulipo. Sasa huo Uhuru ni upi? au unazungumzia swala ya yeye kutangaza kugombea Urais?..

Maana hata hili ukilitazama kwa makini katiba na kanuni za chama chake Majina ya wagombea hupendekezwa na wanachama sio mtu yeyote anaweza kutangaza nia hiyo. Na kati ya majina yalopendekezwa ndipo hupatikana mmoja alowazidi wote kura za maoni. Hii ni demokrasia ya chama na sii matakwa ya kila mtu. Ifike wakati tusome ya kujua uhuru wa katiba na kisheria tulopewa kwa kutumia katiba na sheria za CCM. Na kama unakumbuka Dr.Slaa alipendekezwa yeye kusimama japokuwa hakuweka nia yake ya kugombea Urais. Ni wanachama ndio humchagua mgombea wao kwa mapendekezo yao sio kila mtu anavyojisikia..

Na asikudanganye mtu, kila kiongozi Chadema, CUF au CCM kote kila mtu anataka kuwa RAIS na tusipoangalia vizuri ndio yale ya kuwa na vyama 20 nchini vikigombea kuongoza nchi ilihali vyama vyote vinasimamia Itikadi moja. Vimejitokeza kwa sababu ni watu hawaelewani sio swala la sera kutofautiana.. CDM inataka chama ndio kichukue mamlaka ya kuongoza nchi na sio jina la mtu kwa umaarufu wake kuwaweka Ikulu.
 
If Zitto doesn't violate CDM's constitution or charter, why are you so upset? To be honest with you, Zitto isn't a problem. For, he's been clear and open about what he wants to accomplish, in short and long terms as well. He wants to be the president and he has done his home work.

On the other hand majority of CDM's supporters, probabaly you too, are a real problem. For they have already accepted that Dr. Slaa should be the candidate for the 2015 general election. They believe that Dr. Slaa has a realistic chance to win the election.

Those who have accepted the automatic candidacy of Dr. Slaa are doing exactly what Zitto does. They have advanced the candidacy five years before election. Is this democracy? Absolutely not.
 
Bro whats wrong with you? Did I show any sign of being upset or is it my advice to him? beside I never touched his ambitions til you brought this. People have the say (People's power) who they want to be their Leader and not one person ambition.. Yes, It is democracy as long as some among them want Zitto to lead not Zitto for Zitto... It's not about who stand the change rather peoples choice of who can lead all the people not some of us to accomplish his ambition..Nowhere did I say Dr.Slaa is my choice, or he stand a good chance of winning the coming election.
 
Mkuu ushauri mzuri sana huu.

Hapo kwenye bold:ndiyo msimamo wa wengi wetu humu JF.Hata wale wanaopingana na kauli zake za kutaka urais,haina maana kwamba hawajui kuwa ana haki hiyo.Uliyoyazungumza hapo juu ndiyo haswa wamekuwa wakiyasema wengi wetu humu.Sema ni lugha na namna ya kuexplain,lakini kila anayepinga,nyuma yake ukiwauliza sababu wanakupa hizo hizo ambazo umezitoa hapo juu.

Wengi humu hawasemi kuwa "Zitto hafai kuwa rais",bali wanasema "Zitto anafaa kuwa rais,but...",Yani ni yes,but...
Mkandara,nasikitika kusema kwamba ushauri wako haujazingatiwa."A one man army"

jmushi1, Inawezekana siko peke yangu ninayemfananisha Zitto na Marehemu Frederick Chiluba wa Zambia! Chiluba alikuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja kiasi kwamba unaweza kumkabidhi funguo za gari - regardless!

Zitto ana kila haki ya kutangaza nia yake ya kugombea urais, ni haki yake kabisa. Ila Zitto kama Zitto hana haki hata kidogo ya kusema ni watu wa umri gani wanafaa kushika madaraka. Huu ni ubaguzi (discrimination) na pia ni kinyume na katiba (yetu ya sasa). Lakini pia mimi kama raia kauli ya Zitto naichukulia kama ameingilia uhuru wangu wa kumchagua mtu ninayoena anafaa! Hivi ni waziri mzee gani aliyeiweka hii nchi kwenye giza kama Ngeleja? Amezaliwa lini Ngeleja?

Mwanzoni nilifikiri amenukuliwa vibaya lakini siku kama 3 sasa zimepita na sijasikia Zitto akikanusha kuwa alisema watu waliozaliwa kabla ya uhuru hawawezi kuongoza mageuzi (something similar) yanayohitajika nchi hii! Hii kauli bila kumumunya maneno ni ukosefu wa heshma na inataka kujenga kizazi cha laana. Jamii yeyote iliyostaarabika haidharau watu wazima (ukitaka unaweza kusema wazee). Uzee sio ugonjwa, sio kichaa. Kauli ya Zitto inaibua mjadala juu ya malezi wa 'vijana'. Tanzania imepata uhuru mwaka 1961, mtu aliye na umri wa miaka 62, 65, au hata 75 (kwa tafsiri ya Zitto) huyo anatakiwa akae chini asububiri kufa! Hawawezi kuongoza mageuzi! Ni mara ngapi Zitto amekuwa anachukuwa ushauri toka wa wakina Dr Salim Ahmed Salim, Warioba? Na hao wazungu wanamwanisha kuwa anaweza kuwa rais alishajiuliza wana umri gani?

Labda tujikumbushe, mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi ambapo Tanzania tumepata ahueni baada ya Prof Tibaijuka kuingilia kati. Huyu mama amezaliwa kabla ya uhuru, ana miaka zaidi ya 65, na sasa ndio tegemeo kubwa la Tanzania kwenye huu mgogoro wa mpaka na Malawi.

Mimi binafsi, naamini CHADEMA imejengwa na watu wengi sana Zitto akiwa ni mmojawapo. Lakini kama ungeniuliza jina la mtu mmoja aliyeguza CHADEMA na kuwa kama kilivyo sasa na pengine kubalisha siasa za vyama vingi nitakupa jibu Dr Slaa. Na huyu amezaliwa kabla ya uhuru. (nirudie hapa naongelea mtu mmoja mmoja). Vyama vya siasa upande wa upinzani vimekuwepo kwa miaka 15 wakati Dr Slaa anachukua fomu za kugombea urais. Tofauti ni kwamba tuliona tatizo la upinzani hawakuwa na mtu ambaye wananchi walikuwa na imani naye, mtu ambaye akisema kijiko anamaanisha kijiko, mtu ambaye haishi kwa mtindo wa Maslow Hiarachy.

Nadhani Zitto angetumia busara na kufafanua kauli yake wa wazee. Hayo ya urais ni haki yake, lakini it is not right to condemn other human because of thier age. That is wholly unacceptable.
 
mie naona kama anavyotangaza ndivyo anavyokisaidia chama ili kuwapoteza hawa magamba wajue kuwa kuna mgogoro kumbe ndo mwendo mdundo. tutafika tu, zitto ni rais wangu wa 2035
 
Bro whats wrong with you? Did I show any sign of being upset or is it my advice to him? beside I never touched his ambitions til you brought this. People have the say (People's power) who they want to be their Leader and not one person ambition.. Yes, It is democracy as long as some among them want Zitto to lead not Zitto for Zitto... It's not about who stand the change rather peoples choice of who can lead all the people not some of us to accomplish his ambition..Nowhere did I say Dr.Slaa is my choice, or he stand a good chance of winning the coming election.

Mkandara,

Nothing's wrong with me. I am bouncing just fine. Now concerning what I have said, you might be an exception to the rule. Majority of CDM's supporters, especially here, believe that Dr. Slaa is their candidate for 2015 presidential election.

With regard to Zitto, there's nothing wrong with what he does now. He knows that if he wants to compete, first he must show the intent and second he must position himself.
 
ili kurally behind chadema liwe jambo la maana kwa zitto kwanza inabidi vikao vya chadema viendeshwe kidemokrasia na sio kiubabe ubabe wa mwenyekiti na wazee wa chama.
Chama ambacho katiba yake inasema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi lakini ikifika wakati wa uchaguzi wagombea wengine wanaambiwa wasigombee kwa sababu "they are from nowhere" ukikiendekeza utaishia kuwa tambaa la deki.
waziri samwel sitta aliposema chadema haijawa na watu wa kuongoza dola isipokuwa dr slaa mkamshambulia. Waandaeni watu watakaokamata dola, kupiga kelele ni kitu kingine na kuongoza ni upande mwingine.
 
Kwa tuhuma hizi za uhujumu chama bw. Zitto Kabwe, anguko lake
kisiasa ni dhahiri limefika kama halipo njiani.

Niliwahi kushauri na kusema juu ya Zitto kuutaka Urais watu walinishambulia na kunitusi hadharani, wakati ulikuwa tu ushauri kwa ustawi wa chama chetu .

Tuhuma zinazomkabili zinamuondolea sehemu kubwa sana ya sifa za uongozi hata kama ni kiongozi kwa mwonekano. Nafasi aliyo nayo ya kujirudi au kuzuia uharibu ''damage control'' ni yeye kujitoa kimaso maso bila msaada wa vijana ambao kisiasa ni wachanga na kifikra ni weupe sana.

Zitto anapaswa kuachia ngazi katika uongozi kwa sasa ikiwa ni hatua ya kuwajibika na ku-reset the button. Jitihada zake za kutaka kuona nyumba inaunguka kwa msemo wa 'namwaga mboga mwaga ugali'' zinaweza zizifanikiwe kwasababu washirika wake awaonekani kuwa watu makini.

Ningemshauri Zitto awaase vijana wake wasimwage mpunga kwenye kuku wengi na kukaa kimya ni busara na msaada kwake The only window of opportunity ni yeye kuachia ngazi katika uongozi.

Achie ngazi kwa sababu amedhihirisha betrayal, amepoteza trust na moral authority yake imekuwa severely compromized. Hizi jitihada za kuwatumia immature political gangs kumsafisha zitahitimisha safari yake mapema sana.

Kiwango na umaarufu aliofikia Zitto halafu uangalie timu aliyokuwa anafanya nayo kazi kichini chini ni ushahidi kuwa pamoja na vision na mission anazoonekane kuwa nazo, politically ni immature na ameonyesha poor judgement kama kiongozi. Zitto anahitaji muda akomae kisiasa na hili litabaki kuwa donda ndugu.

Zitto, kama unakipenda chama na unapenda ustawi wa taifa hili, ni wakati muafaka kabisa uweke masilahi yako pembeni kwa kuachia uongozi ili uwe mfano wa vijana shupavu wanaokubali kuwajibika.

Kwasasa huna moral ya kumyooshea kidole Mizengo Pinda ajiuzulu kwa kutowawajibisha mawaziri maana wewe hujafanya hivyo.

Naomba kuwasilisha
 
Mh.Zitto soma na utafakari ila ukweli ni kwamba kama tuhuma hizi zinazokuandama ni za kweli basi huu ni ushauri mzuri kwako na unapaswa kuupokea.Hayo ni maoni au ushauri wangu kwako.
 
Zitto lengo lake ni kung'oka na Dr Slaa, anataka kuja na zile mbinu za CCM za kusema kwa kuwa wote wawili wana makosa inabidi wote wawajibike then baada ya hapo mbinu ya CCM inakuwa imetimia na Dr Slaa hagombei urais 2015 CCM wanapita kiulaini...

Mashambulizi yote dhidi ya Dr Slaa kwa hoja zisizo na ushahidi na ambazo hazimhusu moja kwa moja yameratibiwa Lumumba baada ya watanzania kukataa ghilba za Nape, Shigela na MwiguluChemba. Imewalazimu CCM kutumia mawakala wao wa ndani ya CDM kufanikisha kumuondoa Dr Slaa katika nafasi yake

Zitto hautaki urais na wala hana ndoto ya kuwa rais wa Tanzania, anachotaka yeye ni kumkosesha Dr Slaa fursa ya kugombea urais 2015 kwa gharama yoyote ili kutekeleza mradi wa gharama kubwa wa CCM baada ya kushindwa kupambana na Dr Slaa. Go Dr SLaa Go, watanzania wenye uchungu na nchi yetu tuko nyuma yako na hawa wanafiki wataumbuka kadri siku zinavyoenda na MATUNGURI yao yanaoua hadi PANYA
 
A bit philosophical Mkandara.
Well Zitto ni haambiliki type, kwa nini hawasikii hata ninyi rafikize?
 
siungi mkono hii hoja zitto yupo sawa anachokifanya ni kile anachokiamini kipo sawa hawezi kuwa nyuma ya sera mbovu na mawazo mabovu so nisahihi kusimamia mawazo yake na sikuzote nayaamini yapo sahihi
 
Back
Top Bottom