Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 18,875
- 29,427
Hilo linajukikana, tunachukua tahadhari. Lakini revolutionaries hawafikiri kama wewe. Wao wamejitoa kutetea jamii no matter what happens. Basically wako na falsafa ya Ernesto Che Guevara aliyesema;1. Acha Kuwaamini kwa 100% wale Watu wanaojifanya ni wa karibu Kwako.
2. Tumia ID iliyo anonymous na siyo ile ambayo inakutambulisha Kiuhalisi na wengi wanaijua.
3. Acha kupenda hovyo Wanawake au Wanaume kwani kwa 100% hao ndiyo watatumika Kukumaliza.
4. Hakikisha Mizunguko yako yote ya Siku uwe unaijua Wewe tu na ikiwezekana iwe ni ya Zig Zag Style.
5. Ukiona kuna Watu wanakusifia na kukupongeza kwa uanaharakati wako waangalie mara mbili mbili.
6. Wa Kumkaribisha Kwako awe ni Mama au Baba yako tu kwani Ndugu / Marafiki wengine hutumika.
7. Ukijua unaviziwa ama toa Taarifa kwa Watu mapema na ikiwezekana piga Picha Matukio yote.
Tuwe makini sana na nasisitiza tena tuwe makini mno na namalizia kusisitiza kuwa tuwe makini zaidi Maadui zetu hawalali 24/7.
"I would rather die standing up than to live life on my knees."
Na akaongeza;
"If you tremble with indignation at every injustice then you are a comrade of mine"
Nakuhakikishia huyo Mdude Nyagali hata akiachiwa bado ataendelea kufanya ukosoaji hivyo hivyo. Hata Tundu Lissu ni wa aina hiyo. Hao wamejitoa sadaka kupambana na uovu na hawajali kufa kwa ajili ya kupigania haki.
Kwani Mdude ameshindwa nini kutengeneza fake ID? Alitaka harakati zake zijulikane. Utamfunga jela, utamuua lakini hata wauaji nao huwa wanakufa. Yuko wapi Iddi Amin? Yuko wapi Saddam Hussein?
Ninachoweza kuongeza ni kwamba hizi harakati za mitandao ya jamii zina nguvu sana dhidi ya watawala wadhalimu. Angalia mwenyewe mauaji yaliyofanywa na WATU WASIOJULIKANA kati ya 2016 na 2018 kama vifo vya akina Ben Saanane au Azory Gwanda ni nani waliokomaa kuvikemea kama siyo wanaharakati wa mitandao ya jamii humu JF, Twitter na Facebook?
Na sasa hivi kumetulia hatusikii watu kutekwa na kuuliwa, haya ni matokeo ya kelele zetu kupitia FAKE ID wala siyo kelele za magazeti au TV au Radio. Hivyo vyombo rasmi vya habari vinaogopa na vinatishiwa kila leo na Dr Abbas na Mwakyembe kufuiwa leseni.
Nikuhakikishie kuwa hawa watawala wa awamu ya 5 ni waoga sana ndiyo maana wanatumia fedha nyingi kwenye security yao. Ila kumbuka kama Watanzania wote tunakuwa waoga namna hiyo hawa watu wataingia mpaka bedroom zetu wakabake wake zetu.
Tusiogope kukemea uovu kwa sababu eti watatukamata na kutuua, hata wao watakufa tu