pole zake huyo mdada, yaani hata sijui tumsaidiaje.
kosa ni lake mwenyewe na yeye alikubalije kwenda kanisani kufunga ndoa na mtu ambaye hamfahamu? kumfahamu nina maana kujua current tabia zake. wew unafunga ndoa na mtu eti wazazi ni family friend ndo unasacrifice maisha yako yote? hapo kwa kweli alichemsha.
kwa ushauri tu ni kwamba, ni sawa ndoa ya kanisani haitenganishwi na binadamu, lakini kwa swala hilo anaweza akachukua break kidogo. arudi kwao akatulie, na asali sana kuomba Mungu ambadilishe huyo mume. kuendelea kukaa kwa huyo mume kutamwongezea stress, maana kila akimuona anawaza kuwa nakuja kusimangwa, na hilo la kusimangwa ndo linaudhi sana. Huyo mume kama atamuhitaji basi atajirekebisha na wataendelea kuishi vizuri. umri wake unamruhusu kukaa nyumbani hata kwa 5 years akisubiri Mungu atende Miujiza. asikate tamaa.
Ila kusema ampeleke sijui kwa mchungaji au ndugu au wapi haitasaidia, hilo ndo litabia lake kwa sasa.