anawaza atafanyaje au atatoka vip ndani ya hiyo ndoa
je anaweza kwenda mahakamani ili aweze kusaidiwa ?
msindima kwa imani nguvu ya mungu ipo na inafanya kazi lakini ndo majibu hayawezi kuonekana leo au kesho sometimez inatake time
kuna member mmoja humu anaamini hakuna Mungu, sasa huyo ndio mumeo utamuombea kivipi na yeye haamini? wacheni bwana anaeombewa nae aonyeshe dalili za mabadiliko, sio kuomba tu wakati mtu hayupo huko..........
Mwana F1Hivi lini wazazi wataacha kuingilia maisha ya watoto wao na kuwaacha wachague wenza wao wenyewe? Haya sasa hapo bibie kashaambiwa yeye hakua chaguo lake ata semaje tena?
...Haya mambo kila mkipalangana na mwenzio ndani ukimbilie kushitaki kwa wazee/wazazi, sijui mshenga na wazee wa kanisa mnajidanganya tu...Kama mambo yamewazidi ni nyie wenyewe wa kuamua hatma yenu. Kumbuka hao wazee/wazazi baada ya kikao wanaondoka mnabaki peke yenu wawili na mwenza wako...mh! mnarudi kule kuleee!!! Me i don't believe on this kuwashtakia wazazi....amueni, zungumzeni, mnafikia muafaka na maloveee yanaendelea na kama itakuwa ni pingili basi mtaamua wenyewe kubwaga manyanga...Ni kiasi cha kwenda na kuwaeleza wazazi juu ya tabu hii then wataamua! Unajua ni rahisi kuambiwa amvumilie mlevi kuliko yule aliyetamka kabisa kuwa si choice yake. Otherwise Yeye ndie mvaa kiatu so anajua wapi kinambana zaidi so blahblah za vumilia azipime kwanza na situation yenyewe!!
'Je! watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? Amos 3:3'.
mimi naona mapatano masuluhisho nk yanawezekana tu kama wote wanakubaliana kupatana na kuendelea na ndoa, vinginevyo bora Q apaki mabegi yake aangalie ustaarabu mwingine, sio lazima a file divorce direct, wanaweza kuwa tu separated kwanza halafu Q aangalie hali inavyoendelea na awe tayari kwa lolote, kurudi kwa mumewe kama ataonyesha kubadilika au ku anza mbele kama kuondoka kwake kutakuwa ni sawa na kumnyima punda mbaazi...
Carmel yuko wapi ??
Triplets
Ushauri wako umekaaaa vyema sana na niwakibusara sana na baadhai wa watu nimerishudia hilo likifanyika na wengine hujirudi na wengine husepa mazima no baby come back no more,
Ila kwa huyo sister yangu hapo ipo kazi kweli kweli Kijana ati kasomea Urusi?? Na ndipo tatizo lilipoanzia kwani nami nimeisha fundishwa na walimu wangu wawili kutokea Urusi na ndoa zao zilikuwa na matatizo mpaka twamaliza secondary kweli walimu hao walikuwa walevi kupindukia.
Dada nakuomba umwambie akapumzike kwao kwa muda wajaribu kusuruhisha mammbo kama patakuwa hapatoshi waaangalie ustaarabu mwingine wa maisha yao kila mmoja kivyake period.
Duuhh ni issue nzito sana hiyo
Pole sana kwa ndoa ndoano yako ndugu yangu. Mi nakuomba usiondoke, ila jaribu kutafuta ushauri, hata viongozi wa dini wanasaidia sana katika hali ya namna hiyo, unaweza kumrudia mchungaji aliyewaweka pamoja ukamwelezea yote kisha omba kukutanishwa na mwenzio ili muweze kuangaliana na kusema kwa uwazi, mimi nina hakika maneno matakatifu ya biblia yanaweza mbadili japo kiasi. Maana ukisema uondoke katika ndoa hiyo huwezi jua unaweza kujuta baadae, maana hata rafiki utakayempata ukimsimulia atakwambia wewe sio mvumilivu na hukujaribu kufuata utaratibu kumsaidia mwenzio. Pombe ni kitu mungu alikiumba jaribu ushauri huu, inaweza kusaidia.
kina dada kuna kitu nimekaa usiku kabla sijalala nimewaza sana juu ya huyu dada sijapata jibu
kama mjuavyo ndoa zetu za kikristo zinasema kilichounganishwa duniani na mbiguni kkimeunganishwa hakuna mwanadamua anayeweza kukitenganisha
Swali ...Kama huyo Bibie kwa sasa ana miaka 27 akitoka kwa mmewe itakuwaje kama in future atahitaji kuwa na watoto wake na kiumri bado ni mdogo hataweza kuwa na mahusiano na mtu mwingine na kuyaita mahusiano halali yaani aishi nae kama mme na mke ???
Y kwa nini??
...Haya mambo kila mkipalangana na mwenzio ndani ukimbilie kushitaki kwa wazee/wazazi, sijui mshenga na wazee wa kanisa mnajidanganya tu...Kama mambo yamewazidi ni nyie wenyewe wa kuamua hatma yenu. Kumbuka hao wazee/wazazi baada ya kikao wanaondoka mnabaki peke yenu wawili na mwenza wako...mh! mnarudi kule kuleee!!! Me i don't believe on this kuwashtakia wazazi....amueni, zungumzeni, mnafikia muafaka na maloveee yanaendelea na kama itakuwa ni pingili basi mtaamua wenyewe kubwaga manyanga...
pole zake huyo mdada, yaani hata sijui tumsaidiaje.
kosa ni lake mwenyewe na yeye alikubalije kwenda kanisani kufunga ndoa na mtu ambaye hamfahamu? kumfahamu nina maana kujua current tabia zake. wew unafunga ndoa na mtu eti wazazi ni family friend ndo unasacrifice maisha yako yote? hapo kwa kweli alichemsha.
kwa ushauri tu ni kwamba, ni sawa ndoa ya kanisani haitenganishwi na binadamu, lakini kwa swala hilo anaweza akachukua break kidogo. arudi kwao akatulie, na asali sana kuomba Mungu ambadilishe huyo mume. kuendelea kukaa kwa huyo mume kutamwongezea stress, maana kila akimuona anawaza kuwa nakuja kusimangwa, na hilo la kusimangwa ndo linaudhi sana. Huyo mume kama atamuhitaji basi atajirekebisha na wataendelea kuishi vizuri. umri wake unamruhusu kukaa nyumbani hata kwa 5 years akisubiri Mungu atende Miujiza. asikate tamaa.
Ila kusema ampeleke sijui kwa mchungaji au ndugu au wapi haitasaidia, hilo ndo litabia lake kwa sasa.
ni mahusiano na urafiki wa familia zao ndio uliopelekea yeye na mwenzi wake kuwa wife & husband mwaka mmoja na nusu sasa
Mwanaume alikuwa anasoma urusi -mwanamke akiwa TZ anafanya kazi kutokana na ukaribu wa familia zao na maelewano ..ndipo wakaamua wafanye muunganiko kati ya sistery and brother
mahusiano ya muda mfupi yakafanyika na ndoa takatifu ikafungwa
Sasa ndani ya nyumba mme hashikiki ni mlevi kupindukia anarudi usiku wa manane akirudi home bibie hapewi haki yake na akipewa ni kwa ugomvi na masimango
eti we Q sio choise yangu ni family ndo zilituunganisha imekuwa kama wimbo wa Taifa
Q anauliza je aondoke katika hii ndoa ya masimango au afanye nini