Ushauri: Wapi niwekeze hela yangu ya kustaafu kama Tsh. milioni 100

Ushauri: Wapi niwekeze hela yangu ya kustaafu kama Tsh. milioni 100

Mkuu,kama umestaafu,huna majukumu ya kimaisha kama vile kusomesha etc na unavitega uchumi vya kukuwezesha kuishi basi nakushauri ufanye yafuatayo.

Gawa Pesa yako katika makundi manne:
Kundi la kwanza liwe urithi-
Kundi la Pili liwe sadaka
Kundi la tatu liwe akiba
Kundi la nne liwe uwekezaji

Kwenye Hela ya Urithi weka kwenye T-Bonds au kwenye Fixed deposit ya muda mrefu kutegemea na kiasi cha riba.

Hela ya sadaka tumia kuwekeza katika kutatua changampoto ya kijamii katika eneo lako.Hasa inayohusu elimu au afya.Unaweza kuanzisha NGO yako ukajenga legacy yako nzuri tua kama philantropist.Kuna mahitaji mengi sana katika jamii ambayo yanaitaji watu wenye moyo wa kutoa.Na pia unapojenga NGO yako unaweza pia kupata michango ya wafadhili ili uweze kupiga hatua kubwa zaidi na kusaidia wengi.

Kwenye hela yako ya akiba weka benki tu ili ipate faida taratibu na huku ukiitumia kwa mambo yako madogo madgo kama kununua luku n.k.

Kwenye hela yako uwekezaji hio unaweza ukatumia muda kutafiti aina ya biashara ya kufanya ambayo ina faida nzuri na usiwe na haraka nayo.

Jambo unapaswa kuwa na haraka nalo na la hela ya SADAKA.hilo anza nalo mapema sana na litakusaidia kupata BARAKA nyingi kwa kusaidia wahitaji na kuacha LEGACY katika eneo unaloishi

Nakutakia kila la heri na karibu sana iwapo unahitaji msaada na ushauri zaidi.
Moja ya shauri za hovyo tangu mwaka huu uanze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe hujanielewa.
Nimeongelea bei ya kuuza hapa mjini ni sh 105,000 mpaka 95,000 si 135,000.
Tofauti ya 30,000 mpaka 40,000 kwa pieces moja ni kubwa sana.
Ok.ila pia sio lazima kuuza kwa bei hizo hizo kama wengine na ukamaliza mzigo pia.
Nina ushuhuda watu wanauza baskeli moja 120-180k kwa sehewa na zinatoka haraka mno tena ndani ya mikoa yenye watumiaji wengi wa baskeli na wauzaji wa baskeli.
Sio lazima auzie dar tu
 
Ok.ila pia sio lazima kuuza kwa bei hizo hizo kama wengine na ukamaliza mzigo pia.
Nina ushuhuda watu wanauza baskeli moja 120-180k kwa sehewa na zinatoka haraka mno tena ndani ya mikoa yenye watumiaji wengi wa baskeli na wauzaji wa baskeli.
Sio lazima auzie dar tu
Sawa mkuu inawezekana.
 
Jamani haki kwa sasa ni ipi kwenye soko la pesa..au biashara ya pesa
 
Hakuna sehemu nyingine ya kuweka hela yako Zaid ya kumiliki nyumba za biashara , tafuta location nzuri lipa kiwanja Jenga nyumba pangisha , , kwa baadhi ya mikoa milion 100 unaweza ukajenga nyumba 3 za kupangisha ambapo kila nyumba kwa mwez inaweza kukupa 300k so jumla kwa mwez unaweza kuwa 900k umekosa nn?
 
Njoo ujenge plant ya kuchenjulia marudio ya dhahabu utakuwa unakodisha kwa mwezi milion 4 na gharama ya kujenga plant nzuri ni kuanzia tshs 40,000,000, Kuna miezi plant zinakuwa bizy wateja wanapangwa wakisubiri aliyewahi atoke aingie mwingine
 
Back
Top Bottom