kimweri_wa uzigua
Member
- Dec 15, 2017
- 8
- 8
*BABA MDOGO ANATAKA KUTUDHULUMU NA KIWANJA PIA!*
*Haki itachelewa lakini haidhulumiki*
Baada ya baba kufariki,aliacha mali kadhaa zikiwemo nyumba mashamba viwanja n.k hivi vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa babu,ikumbukwe kuwa babu amezaa watoto wa 3, wa kwanza baba yangu mzazi ambaye ameacha watoto kadhaa ikiwemo mimi,baba mdogo wa kwanza baada ya baba na baba mdogo wa 2.
Baba na baba mdogo wa pili walishafariki,alianza baba late 1990's na baba mdogo 2000s.Baada ya baba kufariki mali zote zilkuwa chini ya babu,nae babu akafariki akamuachia baba mdogo wa kwanza ambaye zimebaki kwenye uangalizi wake kwa kuwa watoto wa marehu kwa kipibdi hicho walikuwa wadogo.Sintofahamu ikaanza huyu baba mdogo kwa kujifanya mali za marehemu kama zake.Iliniumiza sana wakati mama akinisimulia ni kwa kiasi gani ndugu wa mme wake walivyokuwa wanamnyanyasa hivyo hakuambulia chochote pamoja na wanawe
Baadhi ya nyumba na mashamba akauza bila taarifa za wahusika /watoto,kuja kushtuka kashauza.Baadae mama akafariki.Ikawa aliyebaki ni baba mdogo tu na taarifa za mirathi za baba hazijawahi kutoka mpaka leo,hili wacha niweke kiporo kwa sasa.
Sasa ameamua kuja kujenga kwenye uwanja wa marehemu baba ambao walipimiwa na SERIKALI ZA KIJIJI wakati huo,kiwanja kimoja mtu mmoja,hapo kuna uwanja pacha wa baba mzazi na wa babu, namba za viwanja na majina pia ni tifauti,wake ambao kama urithi anavyodai uko chini na wa baba uko juu,yeye amekuja kujenga juu ambao ni uwanja wa kaka yake ambao kimsingi ni urithi wa watoto yaani sisi,mgogoro ukaibuka baada ya watu kuanza kuuliza uhalali wa yeye kujenga kwenye uwanja wetu.Tambo ndo zikaanza akasema mimi sihami hapa pia ni kwangu wala mimi sitambui kama marehemu kaka ameacha mtoto.ikumbukwe baba na mama waliona.
Sasa hivi imekuwa ni vita kati ya watoto na baba yao mdogo,mpaka kumburuza kwenye baraza la kata kumbe huku kote yeye amepenyeza lupia,kwanza kwenye serikali ya kijiji ambako kuna documents za viwanja kuibadilisha taarifa zake sahihi na kughushi,kwa kuwa wazee waliopimaga *VIWANJA* wengi wametangulia mbele za haki lakin amebakia mmoja ambaye sasa anakaaa mbali na hapo nyumbani ikabidi kumfuatilia huko na katika kupeleleza akasema baba yenu alikuj na chochote na kweli amebadilisha taarifa ya kiwanja chenu chote kionekane cha mtu mmoja kwenye serikali ya kijiji.
Mpaka sasa shauri linaendelea kuna tarehe hapo januari limetajwa kusikilizwa.
Kwa hali kama hii naona haki yetu inaendwa kupokwa kwa thamani ndogo ya fedha ya baadhi ya viongozi wa sasa wasiokuwa waaadilifu dhidi ya walalahoi sisi.
*Katika hali kama hii wanajukwa naombeni mawazo yenu nini sisi kama familia tunaweza kufanya ili haki yetu isipotee??*