Ushauri wenu jamani

Ushauri wenu jamani

Siimay

Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
59
Reaction score
12
Assalam aleukum ndugu zangu,nina jambo moja nataka kuliweka hapa japo tusaidiane katika hili!nimekutana na dada mmoja bahati nzuri nakaa nae mtaa mmoja nikatokea kumpenda sana ila cha ajabu huyu mwenzangu baada ya kuanza mahusiano akaanza mizinga mwanzoni nikajua ni ya kawaida tu so sikushtuka sana!anasoma IFM hapa dsm.Sasa juzi kati kanifata anataka nimlipie kodi ya nyumba wakati anajua mi mwenyewe kodi maana bado sijajiweza kiivyo...dizaini nikampotezea basi na yeye akapoteza kingine nikaja kugundua ana mtoto amezaa na msanii flini wa ubongo wa flava cha ajabu siku moja akaniomba hela ya kumlipia mfanyakazi anayemuhudumia mwanae nikamwambia baba yake si yupo?ndo akakasirika kabisaaa...toka hapo akamua kukaa kimya na mimi nikamua kunyuti pia!baada ya kama wiki mbili anarudi na anaomba msamaha mi nikacheka nikamwambia bwana mi na wewe tuachane kwa amani maana kama hatutaweza kuwa pamoja kabisa!ila anasisitiza tu...ushauri please!
 
You are not serious!
Shida yako bado unamtaka huyo dada, ungekuwa makini kibuti moja tu ni once and for all!
Huo ni mtambo wa Matatizo achana nae mbali Broda!
 
Acha ubahili wewe,wenzio wanahonga hadi magorofa,we unaona noma kuhonga kodi ya nyumba?
 
temana naye atakuzidishia majukumu bure!
 
Mi nakushauri ukae nae mbali kwasababu tu hakukwambia kwamba ana mtoto wakati mmeanza kuwa pamoja. Kunavitu vya kuficha ila.hicho sio kimoja wapo.
 
Mi nakushauri ukae nae mbali kwasababu tu hakukwambia kwamba ana mtoto wakati mmeanza kuwa pamoja. Kunavitu vya kuficha ila.hicho sio kimoja wapo.

Kuficha mtoto au watoto ni mbaya sana.
 
kwani hiyo kodi na hayo matumizi ya malezi ni shing ngapi..!??
 
Kuficha mtoto au watoto ni mbaya sana.

Sijui watu hua wanaogopa nini au kwanini wanawaonea watoto wao aibu!!!?

Kuna mmoja alimficha wake mpaka anaolewa baada ya miaka minne ya ndoa ndio mume anajua yule anaemuitaga mkewe shangazi ni mwanae.
 
Unataka matatizo yake amwambie nani mtu wake wa karibu?..mimi nadhani inshu hapo labda kama hauna uwezo wa kumsaidia matatizo yake lakini sio swala la kumwita mpiga mizinga.Iwapo unamueleza ukweli kuhusu hali yako kifedha na bado hakuelewi then inategemea kama mna malengo ya muda mrefu au ni wale wakumaliziana shida zenu tu,kama mna malengo ya kuishi pamoja tayari kutakuwa na gap kubwa sana katika mahusiano yenu ambayo yatapelekea msifikie malengo yenu.Nadhani umeshaamua kwa kuona kwamba umuwezi kwa kuwa anamahitaji ambayo uwezi kumtimizia hivyo kuwa pamoja mtakwazana tu....chapa lapa mkuu.
 
nafikiri mngefikiria mapenzi kwanza...je mnapendana? na kama mnapendana basi lazima mtajikuta mnatengeza mazingira mazuri baina yenu....! sasa basi hili litakua ni jukumu lenu wote wawili (kodi ya nyumba, na huyo mtoto) inabidi muongee vizuri jinsi ya kutatua mambo hayo na kuendelea na maisha!
Lakini kama alikua ni demu wa kuzugia tu...na una uhakika mapenzi kwenu ni kitandani tu! aaaah potezea tu coz mwisho wa siku mtaishia kupotezeana muda, hela na lawama kibao..!
 
Hivi hawa watu wanaosemwa kila siku hapa JF wao hawapo hapa JF?????
 
duh mkuu huyo hakufai sababu anaonekana ni wale wanao-capitalise kwenye mahusiano aka wachunaji....na wewe unasema huna pa kuchunwa...hata ukilipa hiyo nyumba kesho atakuja na jingine....ungekuwa uko fresh ningeshauri umsaidie tu maana tayari ni single mother huyo alafu mwanafunzi...kwa hiyo kimsingi hapo mizinga ipo sana sasa amua moja...kuhudumia kwa roho safi kwa hicho kidogo ulicho nacho au kutoka nduki...
 
wanawake nao jamani wanajidhadhalisha mno. kwani alivyopanga nyumba aliagana na nani atamlipia kodi ya nyumba! nyumba yako mwenyewe kwenye kodi umkabe mwingine. hebu achana nae huyo, tena muogope kama ukoma. Kesho atakuambia ana kiwanja umnunulie.
 
Back
Top Bottom