Ushauri wenu: Kuna umuhimu kuridhisha wakwe wa siku hizi?

Ushauri wenu: Kuna umuhimu kuridhisha wakwe wa siku hizi?

Mkuu achana na watoto wanaoponda uzi huu kiukweli wakwe wengi wanachangia kuvunja ndoa za watoto kwa masrahi binafsi .
 
Wakwe zako hao especially mama ni nomaa. Pole sana. Wamezingua kusema kweli.
Ila namuelewa mkeo kuwakingia kifua wazaz wake saabu nae hawez kuonyesha chuki hadharani kwa wazazi wake.
Inawezekana nyuma ya pazia alimsema mamaake ila ndoivo hawez kuonyesha waziwazi kua walizingua big time.
 
Nimekusoma bro na nakupa pole kwa yote,ila ushauri wangu kwako samehe yote,na muanze upya,ukisamehe mungu nae atakusamehe makosa yako na utaishi kwa amani,ukiendekezq chuki utaugua ugonjwa mbaya ambao hatimae,utapata maradhi yasiyotibika.maisha ni changamoto na utu na ubinadamu ni namna tunavyokabiliana na changamoto hizo
 
mchumba asomeshwi!!
nyumba haijengwi ukweni.
ndio sela zangu mm.
nabakia mm na mke wangu n watoto wangu.kwa afya ya familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah pole sn kwa misukosuko kaka, sisi tulio kwenye ndoa tunaelewa unachokipia. Ni shida sana kuwa karibu na wakwe. Ni bora kuwa mbali nao kbs. Hapo upo sawa kabisa kwa ulichokifanya kutokwenda tena wala kutokua na story nao. Next time kumbuka ni marufuku kujenga ukweni
 
Back
Top Bottom