Ushauri wenu kwenye kuagiza hii gari wakuu.

Ushauri wenu kwenye kuagiza hii gari wakuu.

Gari la nini lote hilo babu? Chukua KI-IST chako au Carina kwa misele michache ya mjini then pesa nyingine kama uko nayo nyingi chukua ushauri huu na uje unishukuru kwa bata utakalo kula hapa nchini

[emoji116]
Nunua Honda Africa Twin motorcycle 1250cc

Yamaha Super Tenere 1200cc/ 700cc

Anza kua mtalii wa ndani,kitu inakutoa Dar to Arusha chap kama ulikuwepo,unakula vyako then chap unazama Mwanza kwa mwendo wa ndege unakula SATO tuliiiiivu kabisa ukiwa huna haraka kisha chap unageuka Dar kama ulikuwepo kitaa kumbe umevuka mikoa

Ya nini ligari lote hilo ambalo analo kila mtu mjini mpaka tubinti tudogo twa bank huko tumebeba mkopo tukanunua na wewe unafata ushauli jf kweli kwa gari lenye kubugia mafuta

Nisamehe kama umekwazika lakini hilo ndo bata la kweli.

View attachment 1712847
Sijawai ona mpumbavu kama wewe.....yaani nani kakwambia interest ulizonazo wewe, kila mtu anazo .. we kupenda pikipiki unahisi kila mtu atapenda??? ...eti nunua ist ??? Unaweza kuta uwezo wa jamaa financially ni mara tano yako suala la mafuta kwake sii ishu kabisa we unakuja na mawazo yako ya kimaskini eti yanini gari kubwa linabugia mafuta... mi naona we unafaaa hata kupigwa kofi uamke kwenye uo ujinga ulionao.....iko hivi mpaka jamaa kataka harrier hilo ndio chaguo lake na lazima liko ndani ya uwezo wake... we ulichotakiwa ni kumsaidia alichoomba kama una uzoefu kama huna au hujui kausha sasa badala yake unakuja tena kumpangia upuuzi wako mara kila mtu analo mjini na si ajabu utakuwa mtoto kuna utoto utoto nauona hapo.
 
mshana naomba unieleweshe hyo CIF na mm nipate hyo elimu inaweza kunisaidia

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
Mimi sio Mshana ila naweza kujibu.

CIF ni gharama ya kununulia gari, kulikagua na kulisafirisha hadi bandarini nchini kwako.

Kwa mfano, gari inauzwa USD 2000, gharama za usafiri (freight) 1000 USD na preshipment inspection 300 USD jumla ni 3300 USD. Kwa hiyo ukinunua gari hii ndio pesa unayowalipa wauzaji kule japan na wao wataituma gari.

Ikifika ndio gharama nyingine za ushuru, port charges, wharfages, shipping line etc zitalipwa hapa na utatoa gari yako.

Hii ni kwa anaeagiza gari sio anaenunua showroom
 
Back
Top Bottom