Tunza hiyo laki moja yako na anza kufanya kazi kwenye godauni huku unapunguza matumizi yake baada ya muda ukifikisha laki 3 au nne ndio unaanza kuuza nguo lakini tena sio wewe unampa mtu ambae anaweza kukuuzia huku ukiendelea na biashara ya godauni, biashara ya nguo ikianza kuchanganya ndio unaweza kuacha kwenye godauni na kung'ang'ania kwenye nguo, tofauti na hapo unaelekea kufeli mtaji wa laki moja ujue kunachangamoto kibao katika hilo na unawashindani ambao wapo kwenye hiyo kazi kitambo lazima uingie kwa kujipanga, lazima utauza nguo zote lakini inaweza kuwa nguo moja kila baada ya siku nne au nguo nyingi kwa bei ya hasara. chukua uamuzi sahihi