Ushauri wenu ni muhimu

Ushauri wenu ni muhimu

love peace

Senior Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
130
Reaction score
37
Wakuu,kati ya kufanya biashara ya kuuza nguo vyuoni hapa Dar kwa mtaji wa laki moja,na kufanya kazi kwenye godauni kwa mshahara wa laki moja kipi ni chema hapo jamani?

Nishaurini wakuu.nahitaj msaada wenu.
 
ukisubiri mshahara wa godawn itakula kwako..kwa siku utaingiza si zaid ya 3500
kachukue nguo za bukubuku(za kike/watoto) utauza kwa elfu 2 mpaka 25 au kajumue cd za kizungu faida kwa siku ukiuza cd 10 ni elfu 10 au zaidi hapo ni kukaza na utatoka ukiwa na mipango mizuri na hela utakayozalisha
 
Tunza hiyo laki moja yako na anza kufanya kazi kwenye godauni huku unapunguza matumizi yake baada ya muda ukifikisha laki 3 au nne ndio unaanza kuuza nguo lakini tena sio wewe unampa mtu ambae anaweza kukuuzia huku ukiendelea na biashara ya godauni, biashara ya nguo ikianza kuchanganya ndio unaweza kuacha kwenye godauni na kung'ang'ania kwenye nguo, tofauti na hapo unaelekea kufeli mtaji wa laki moja ujue kunachangamoto kibao katika hilo na unawashindani ambao wapo kwenye hiyo kazi kitambo lazima uingie kwa kujipanga, lazima utauza nguo zote lakini inaweza kuwa nguo moja kila baada ya siku nne au nguo nyingi kwa bei ya hasara. chukua uamuzi sahihi
 
Kama una mahali pa kuishi kauze nguo. Baada ya miezi michache kama utakuwa na nidhamu ya fedha utaweza kuwa na kipato kinachozidi laki 2. Huna haja ya kwenda kufanya kazi kwenye godauni ili udundulize kuongeza mtaji. Mtaji huo huo wa laki utajiongeza wenyewe huku ukiendelea pia kujiongezea uzoefu kwenye hiyo biashara yako.
 
Back
Top Bottom