Ushauri wenu unahitajika katika biashara hii

Ushauri wenu unahitajika katika biashara hii

Gluk

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
1,859
Reaction score
3,008
Habari zenu wanaJF
Lengo la uzi huu ni ukuomba msaada wa mawazo pamoja na ushauri wa hiki ninachofikilia kukifanya, maana naamini humu kuna watu tofauti.
Nadhani katika pitapita zenu mmekutana na wale vijana wauza aidha dawa za mswaki, Sabuni, vyombo huku wakiongea maneno yenye ushawishi sana kwa kuelezea kuwa wanatokea katika kampuni fulani.(biashara ya promosheni )
Nimekuwa na wazo hili zaidi ya mwaka mmoja ila sijui pa kuanzia mpaka kufungua kampuni ya namna hiyo ili niweze kutoa ajira kwa vijana wenzangu ili tusaidiane maisha.
Naomba kujua pa kuanzia nikimanisha ni mamlaka zipi zinazohusika na hiyo biashara,
changaomoto zake na ushauri mwingne pia nitaupokea asanteni sana.
NB:mtaji si tatizo upo wa kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla sijakushauri,labda nikuulize kitu..hicho unachotaka kukifanya/hiyo nia yako ya kufungua kampuni ya kuuza bidhaa mbalimbali ni kitu unachokipenda kwa dhati ya moyo wako??au umeona ufanye tuu kwasababu mtaji upo wa kutosha??

NB: ni dawa ya(za) meno na sio mswaki.
 
Ni kazi ninayoipenda kutoka moyoni ndo maana napenda niifanye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jioni nitakuibia siri

[emoji252] [emoji479]
 
Aisee... Unakuwa na bidhaa afu unakuwa na timu ya machinga wa kuzitembeza!
 
Umeshawaza collateral ya hao vijana? Manake waswahili ugonjwa wetu mkubwa ni uaminifu. Wasije wakachukua wakatoweka.

Kuhusu authorities, nadhani kwa sababu hauzalishi bidhaa unahitaji leseni tu ya manispaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeshawaza collateral ya hao vijana? Manake waswahili ugonjwa wetu mkubwa ni uaminifu. Wasije wakachukua wakatoweka.

Kuhusu authorities, nadhani kwa sababu hauzalishi bidhaa unahitaji leseni tu ya manispaa

Sent using Jamii Forums mobile app
kuhusu uaminifu hilo nitalizingatia kwa ukaribu sna, asante sana kwa mwongozo wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom