Ushauri wenu wa ki daktari wakuu

Ushauri wenu wa ki daktari wakuu

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Wakuu kumekucha!
Naombeni ushauri wenu yaani saa hivi kila asubuhi nikiamka napiga chafya sana!!!vipi wakuu huu ni ugonjwa niwahi aghakhan au!!!
 
Chumba, madirisha, dari hayana vumbi? Vipi hali ya hewa, baridi au upepo?
 
Mkuu ndani hakuna vumbi ila upepo upo na mazingira ni mazuri
 
Fua mashuka yako kila baada ya siku tatu, utapona kabisa. Unajifunika ama kulalia shuka chafu labda
 
Mkuu hicho chumba kitakua na vumbi na shuka pamoja na mito unayolalia vitakua vichafu..
 
Hapana mkuu huanabadilisha kila baada ya siku tatu[emoji134] [emoji134]
 
Wakuu kumekucha!
Naombeni ushauri wenu yaani saa hivi kila asubuhi nikiamka napiga chafya sana!!!vipi wakuu huu ni ugonjwa niwahi aghakhan au!!!

So mtu akipiga chafya ndo anatakiwa aende aghakhan??..why aghakhan?
 
Pole!! Uwezekano mkubwa ni kwamba kutakuwa na kitu kinachoku-irritate puani ndio maana unapiga chafya asubuhi. Hicho kitu kinakuwa kimejikusanya kwa kiwango kikubwa usiku mzima. Hakikisha chumba ni kisafi vya kutosha bila mavumbi (dusty) na kwamba mashuka au blankets nazo ni safi.

Je unalala ukiwa umefunga madirisha? Kama jibu ni ndio na haita hatarisha usalama wako nashauri ulale ukiwa umeacha dirisha wazi. Kwa maana ya kuruhusu mzunguuko wa hewa. Hewa iweze kuingia na kutoka chumbani kiurahisi.

Na je vipi kuhusu maji ukiyaingiza puani...bila/na sabuni? Wakati mwingine hili nalo linaweza kutokea....chunguza vizuri ujue kinachoku-irritate ni nini ili ukiondoe/ukishughulikie kwa kadri utakavyoweza au utakavyoshauriwa na daktari.

Uwezekano mkubwa ni kwamba una allergy na dusty/vumbi au kikemikali fulani humo chumbani mwako au kwenye maji kama nayo yanakusababishia tatizo hilo ukiyaingiza puani. Nenda hospitali upate ushauri muafaka.
 
Nashukuru mkuu nitafanya hivyo!!ubarikiwe sana[emoji122] [emoji122]
 
Back
Top Bottom