Ushauri wenu wakuu kabla sijachikua maamuzi magumu ya kuuwa!

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Wakuu poleni na weak and
Mimi nina rafiki yangu wa karibu sana!! Yaani ni mtu wangu wakaribu sana kiasi kwamba chake changu na changu chake!

Sasa wakati leo naelekea zangu stendi gafla nikakutana nae yeye kaongozana dada mmoja!sasa mimi tukasalimia fresh wote tukamaliza!sasa mimi nikamvuta yule rafiki yangu pembeni nikamuuliza vipi huyo ni dadaako??

Wakuu kwa kweli sikuamini yule rafiki yangu kanipiga kofi hadi nikapatwa na kizunguzungu!!mpaka sasa nijiuliza hivi pale kosa langu ni nini!!!wakuu naombeni ushauri wenu kabla sijachukua maamuzi magumu kwa huyu rafiki yangu!!!
 
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe usipende kuuliza uliza yasiyokuhusu, vuta subira mtu afunguke kama anaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

 
Nenda polisi kachukue PF3 ukatibiwe ...hayo ya kuua kwa ajili ya kofi ni ujinga , kama vp mpotezee tu
 
1. wa stendi na @k 4real ninyi ni watu ambao post zenu nazihusudu sanaaa..[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
2.hakuna haja ya kuua wala kuchukulia hasira, 100% jamaa alichukizwa na swal lako. Cha msingi onana nae umuombe msamaha na mmalize tofauti zenu
NB:KUMBUKA WW NDO UMEANZA UCHOKOZI
3.Nimemis zile post zakk za helicopter na raman ya dunia..[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe usipende kuuliza uliza yasiyokuhusu, vuta subira mtu afunguke kama anaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Mkuu huyu Kofi tuu anataka kuua, angejiuliza aliyotendwa na nchi hii chini ya chama cha majipu kwa miaka 50 angewatafuna kabisa
 
Unasema mtu wako wa "karibu sana", unasema "chake chako" halafu mwanamke aliyefatana nae hujuwi kama ni dada'ke au la?

Kwa hayo tu nnadiriki kusema kuzabwa kofi ilikuwa ni haki yako. Maana hujijuwi hujitambuwi.

Punguani wahed.
 
Sasa wakuu kuuliza tuu ndo anikate kofi kiasi hicho au alikuwa na lake jambo maana nimefikiria mara mbili mbili hadi nikaenda kunoa panga!
 
Sasa wakuu kuuliza tuu ndo anikate kofi kiasi hicho au alikuwa na lake jambo maana nimefikiria mara mbili mbili hadi nikaenda kunoa panga!
Pigwa garagazwa kabisa. Ujuenini! Ww ni muongo %100. "Chake chako&chako ni chake". Pata somo'apo. Jamaa alishagundua ckunyingi kuwa chako ni chako na chake ni chako. Pale ulimuita kumzingua ili uendeleze ufisadi wako. Kwanini hukufanya subira kumuuliza muda mwingine tofauti na hapo?:Kahuni.Kakurud, umpende na ujirekebishe.
 
Muuaji aombi ushauri kama wewe lala ukiamka hasira zimeisha
 
Ilitakiwa akuongeze na ngumi 3 moja ya kifua na mbili za uso!
Inaonesha kuna kitu kingine ulifanya zaidi ya kuuliza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…