Ushauri wenu wana jf

Mocrana

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
536
Reaction score
122
nashindwa niamue lipi, uhusiano una miezi saba, unagundua mwanaume uliyenaye ana mke wa kurithishwa baada ya kaka yake kufariki, mwanzo wakati mnaanza umemuuliza kama kuna kitu chochote ambacho anatakiwa kukuweka wazi akasema hakuna, sasa unakuja gundua hilo, tena baada ya kukuta picha nyuma imeandikwa wife na picha za watoto, tena anakwambia kati ya hao watoto mmoja wa kwake, na hapo baada ya kumbana ujue ukweli wote, sina uhakika kama huo ni ukweli au la, mana kwa sasa nahisi kutokumuamini tena, naombeni ushauri wenu jamani.
 
Hv bado wanawake wanarithishwa? Na wao wanakubali kabisaaaa???
 
Ushauri gani mungu kakuonyesha mapema chapa rapa!
 
pole sana, hapo kama hukuwahi kufikiria kuwa mke mdogo bora ujiondoe tu!
manake hapo si mahali pako tayari kuna mwenyewe
 
si umuache kwani mwanaume ni huyo huyo mmoja?
 
Kwani we tatizo lako nini kama anakupenda na anakuridhisha?.. Si bora kushea penz na mtu unayemfahamu kuliko viruka njia wa mtaani.. Au unamtegemea jamaa kwa kila kitu unahisi huyo mama na wanawe watakupunguzia share?..acha ubinafsi bana..after all siku hizi wanaume halisi ni scarce resource..
 
Mocrana hio ni bonge la Cross roads.... I can Imagine maumivu wapata juu ya kuja tambua hilo, Natambua pia hope ambayo wajipatia somewhere ndani ya roho yako kua itakua kweli akupenda ndio maana amekuficha... Ukijifariji kua anakuhitaji wewe zaidi kuliko mke wake na mambo mengine kibao! The next step to take inategemea mambo mengi saana.... Na kabla hujaamua la kufanya kuna mambo ya kuzingatia...

Kama mna mahusiano ya mda huo na hukutambua na mwaelekea mwaishi pamoja; taratibu zipo vipi? Kua akirithishwa anaruhusiwa kuoa mke ambae kampenda na kumchagua mwenyewe? Una hakika sio tu kwamba anajitetea na anataka kua na wewe; akijua kwa kukwambia alilazimishwa na babake atapata huruma yako kua hampendi huyo mwanamke (hapa usijidanganye; kitendo cha kutembea na picha na kuandika my wife na watoto ni dhahiri ampenda mno!). Una Umri gani? Kama sio less than 24 huyo kaka/baba anakuzibia riziki ni wa kumuacha na kutulia hadi utapompata ambae ana kufaa....

La kuzingatia.... Sioni ubaya Kaongopa (kuna mambo mengine Mpenzi wako huwezi mwambia) ila hilo sio la kuongopa.... Ilitakiwa awe wazi toka mwanzo. Nakutakia kila la kheri katika maamuzi yako.
 
Mocrana, sijui kama utanielewa ila soma kwa makini haya,

nijuavyo mimi mke wa kurithishwa kwa maisha ya siku hizi huwez kulla nae kama mke ila tu unachokifanya ni kuwa msimamiz wa ile familia kwani bado watu wanamentality kuwa mwanamke bila nguzo ya mwanaue hawezi. Kama mumeo alikipanda kwa bahati mbaya kitanda cha ndugu yake na kupata mtoto ilihali nduguye ni marehe basi huyo inabidi awe mkwe kwa kua kimila yeye ndiye msimamizi wa huo mji. Wewe sijui kama ni mke wa ndoa au unaishi uchumba sugu na huyo bwana, kama ni mke wa ndoa basi huwez kuondoka kwani ili uondoke lazima either iwe umemkuta katika uzinifu kinyume chake that is your cross. suluhisho. ongea naye japo huna imani naye ili akwambie nii msimamo wake na ukiona kuwa hupati majibu ya kuridhisha omba ruhusa nenda kwenu kwa siku kama 14 hivi usimweleze mtu yyte bali jiangalie kama kweli utaweza kuish bila yake ( hapa unapima moyo wako unampenda kiasi gani ) ukiona unamkosa sana basi rudi manake huna ujanja.

Kama mnaish uchumba sugu basi usipate shida haawara hana talaka.
 
simtegemei kwa chochote nina fanya kazi na ninalipwa vizuri sijawahi omba hata senti kwake
 
ahsante dada Asha yes anaruhusiwa kuoa anayemtaka, as for umri am in early 30's, na huyo mama ana mtoto mwingine wa miezi 10 ambaye amezaa na mtu mwingine aliyezaa nae yeye ana miaka 6
 
thanks kwa ushauri wako
 
Kama huyo mtoto wa miezi kumi sio wa mpenzi wako bali wa mwanamme mwingine, inaonekana hawana mahusiano ya mme na mke halisi.

Labda shemeji aliamua kumpoza mke wa marehemu kipindi cha Eda wakajikuta wametiana mimba.

Sikushauri umwache haraka, fikiria kama unaweza ishi na mme aliyezaa na shemeji yake na labda ndio anamtegemea kwa kusapoti famillia ya marehemu.

Mahawara hawaachani.

ahsante dada Asha yes anaruhusiwa kuoa anayemtaka, as for umri am in early 30's, na huyo mama ana mtoto mwingine wa miezi 10 ambaye amezaa na mtu mwingine aliyezaa nae yeye ana miaka 6
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…