nashindwa niamue lipi, uhusiano una miezi saba, unagundua mwanaume uliyenaye ana mke wa kurithishwa baada ya kaka yake kufariki, mwanzo wakati mnaanza umemuuliza kama kuna kitu chochote ambacho anatakiwa kukuweka wazi akasema hakuna, sasa unakuja gundua hilo, tena baada ya kukuta picha nyuma imeandikwa wife na picha za watoto, tena anakwambia kati ya hao watoto mmoja wa kwake, na hapo baada ya kumbana ujue ukweli wote, sina uhakika kama huo ni ukweli au la, mana kwa sasa nahisi kutokumuamini tena, naombeni ushauri wenu jamani.