USHAURI: Zanzibar Heroes iwe ndio timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars)

bitekutecha

Member
Joined
Nov 5, 2017
Posts
15
Reaction score
6
Nimejaribu kukiangalia kikosi cha zanzibar kwenye michuano ya kombe la chalenji inayoendelea nchini kenya ambako timu yetu ya Kilimanjaro stars imeambulia patupu, ninashauri kocha wa Stars ateue kikosi kizima cha Zanzibar kilichotinga nusu fainali kiwe ndio Taifa Stars yetu, hii ni kutokana na uwezo mkubwa iliouonyesha katika michuano hiyo hadi kufikia hatua cecafa wameamua kuwapima mkojo wachezaji wake kubaini kama wanatumia dawa za kuongeza nguvu.
 
Hahahaaa wewe hujui kwanini wazenji ni bora. Hawa wachezaji wengi wanacheza bara, hawa wana vipaji walipaswa kucheza bara kama professionals. Ni sawa na bara wangewachukuwa mf. Samatta wangefanya vizuri. Nashauri ZFA waangalie suala la michezo lisiwe la muungano ili waZNZ wawe professionals kule bara.
 



Hoja yako haina tofauti na ile hoja inayotolewa na wenye expansion joint ya ubongo wakipendekeza jpm aongezewe muda wa uongozi!
 

Kwani hao si Pía wanatumika Taifa stars kwenye Mechi za Afrika ? Au Kama mtoa maoni wa awali, hicho kikosi kiwe Cha Taifa stars !!! Au ndo nawe unaona Zanzibar kuwa ni nchi ??
 
Naunga mkono hoja , Ila kocha wao ndio aendelee kufundisha .
 
Hata mimi nawaza Hivyo. Waboreshe kidogo tu. Waongezwe samata na Msuva Pale mbele, Himidi Mao hapo kati na Manula asaidiane Golini na huyo kipa wa Zenji......
 
Kwani toke lini Michezo ilikuwa suala la Muungano?
 
Tutaona kama mtacheza CAF.
Hujajibu swali, Tokea huo Muuitao muungano uanzishwe Michezo sio suala la Muungano, lakini kwa kujidai ujanja wenu Tangnanyika ikajidai kua ndio Tanzania ikawa Hela zote za kukuza michezo kutoka FIFA munazila nyinyi tu
 
Kutokana na umahiri na ushujaa mkubwa pamoja na mafanikio ya timu ya taifa ya zanzibar nimewaza tufanye hivi; Timu hii na kocha wake pamoja na jopo lote la ufundi wapewe nafasi na ndio iunde timu ya taifa ya Tanzania-Taifa Stars. Nimewaza hivi kwasababu hii ni nchi moja na inapofika ushiriki wa mashindano makubwa zanzibar haihesabiwi. Ni kweli watanzania tunakiu ya mafanikio katika soka, lakini tunafanikiwaje? Hebu tuitumie timu hii kama Taifa Stars, labda hii inaweza kuwa fursa kwetu. Naamini hatuhitaji majina makubwa ili kushinda, TUNAHITAJI WACHEZAJI WANAOELEWA NA KUTAMBUA KUWA ZAIDI YA WATANZANIA MILIONI 45 WANAWATEGEMEA NA KUWAAMINI WATU 30 TU ILI KULILETEA SIFA TAIFA- HATUHITAJI WAPIGA PESA WANAOTANGUZA TAMAA BADALA YA KAZI, tunahitaji nia na malengo na kujituma. Kama majina makubwa tulisha yatumia sana lakini mafanikio ni sifuri. Nakaribisha maoni, povu, matusi vyote ruksa!
 
Kwa kweli vijana wa Zanzibar Heroes wamebadilisha mtazamo wa soka wa visiwani, wengi walikuwa wakiidharau hii timu lakini mafanikio yake yamedhihirisha kuwa wazanzibari mpira wanaupenda na wanaujua kuucheza na wana moyo wa kujituma hata kama hawana motisha kwenye soka lao. Kwa kuweza kufanikiwa kucheza fainali kwenye CECAFA inabidi wapongezwe na ikiwezekana wapewe na zawadi kwa kufika hatua hiyo hata kama hatashinda fainali.
FAT inabidi itazame jinsi ya kuunda timu ya taifa kwa kuwashirikisha wanzibar ili tupate kupiga hatua kwenye soka letu la Tanzania.
Ni vigumu Zanzibar Heroes kuwa ndiyo timu ya Taifa ya Tanzania lakini wachezaji wake wengi wachukuliwe kwenye kikosi cha timu ya Taifa. Ikiwa haiwezekani basi Zanzibar ijiwakilishe yenyewe katika mashindano ya kimataifa si kwa CECAFA peke yake.
 
naona huu uzi hauna wachangiaji,wengi hapa ni watanganyika hamsemi kitu uchungu mtupu,jikazeni basi miaka ijayo mshinde nyie
 
Nani alie kwambia suala la michezo ni la muungano? taifa stars kujitia fifa na cap ni kinyume cha katiba na mkataba wa muungano, tatizo lilopo wabunge wa ccm zanzibar na cuf wameshindwa kuhoji uhalali wa taifa stars kujitia fifa.
 
Wazanzibari tunataka kusimama kama zanzibar na Tanzania tanganyik
 
Matusi hayo!
 
Serikali ya Zanzibar, raisi wake ,mawaziri wake, wawawakilishi wake ,wote kimya wanashindwa kuipongeza Zanzibar Heroes kwa kogopa kutumbuliwa na Magufuli

Aibu kubwa sana kuwa na viongozi ambao wako madarakani kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa sio maslahi ya taifa wanaloliongoza
 

Wazo zuri ni Tanganyika ijisajili kwenye vyombo vya michezo vya kimataifa kwa jina la "Tanganyika" sio la Tanzania ili Zanzibar nayo iwe na uwezo wa kushindana kimataifa...mbinu hiyo imetumiwa na England,wales na Skotland kwenye mungano wao wa United Kingdom..

Kumbuka kuwa mungano wa United Kingdom.. umefanana na huu mungano wa Tanganyika na Zanzibar,wao wameungana nchi tatu England,wales na Skotland na zote zinashiriki kwenye michezo ya kimataifa yakiwemo ya FIFA,Mungano wa Tanzania tumeungana nchi mbili lakini inashiriki nchi moja tu
 
Kama mlikuwa hamjui ndio mnatakiwa mjue kuwa zanzibar toka zamani kiuhalisia ina vipaji vingi sana vya mpira.
Ukiwaona unaweza kuwadharau lakini wanakuaibisha mbele ya macho yako
 
Kama mlikuwa hamjui ndio mnatakiwa mjue kuwa zanzibar toka zamani kiuhalisia ina vipaji vingi sana vya mpira.
Ukiwaona unaweza kuwadharau lakini wanakuaibisha mbele ya macho yako
Hiyo ni kweli kabisa mi nimecheza mpira na wapemba wakati mdogo, yaani jamaa mpira uko kwenye damu kabisa na hata kichwani wapemba wapo vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…